07-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Itikadi Ya Mashia Kuhusu Vitabu

 

Bila shaka wislamu wote wanaamini kuwa Qur-ani ni kitabu cha mbinguni kilicho teremswa kutoka kwa Allah kuja kwa nabii wake Muhammad bin Abdillah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Lakini nilipatwa na mshangao mkubwa sana baada ya kusoma kwangu na kuvipitia vitabu vyetu vya kishia ambavyo ndivyo vinavyo tegemewa kama marejeo yanayotegemewa, nilikuta majina ya vitabu vingine ambavyo vinazingatiwa kwa itikadi ya kishia kuwa navyo ni vitabu vitukufu ,na wana zuoni wetu wakubwa wa kishia wanadai kwamba vitabu hivyo pia viliteremshwa kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja na Qur-an, na vitabu hivyo alibaki navyo Amiril-muuminina Ali bin Abi talib.

Wala hakuvibainisha kwa watu yeye Ali wala mtume na huu ni uzushi wa mashia wanaomzushia Ali.

Na vitabu vyenyewe ni hivi:

1-ALJAAMIA (Mkusanyiko wa elimu)

Imepokewa kutoka kwa Abi buswair kutoka kwa Abii Abdallah alisema: mimi na Muhammad, sisi tuna kitabu kinachoitwa Aljaamia, je, ni jambo gani litakalowafahamisha wao ni nini hiyo Aljaamia? Akasema kumuambia mtume  nimejitowa muhanga kwa ajili yako , nifahamishe ni nini hiyo Aljaamia?  Akasema ni sahifa kitabu chenye urefu dhiraa sabini kwa dhiraa za mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kitabu hiki ni maneno yatokayo mdomoni mwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na kuandikwa na Ali bin Abitalib kwa mkono wake, ndani ya kitabu hicho kumebainishwa halali na haramu na kila kitu wanacho kihitajia watu katika maisha yao ya kila siku, hata wadudu walio chini ya ardhi.  kwa kuthibisha hayo angalia: Al-Kaafi juzuu ya kwanza uk. 239, na Bihaarul Anwaar juzuu ya 26 uk. 22.

Na kuna riwaya nyingi sana zinazoeleza habari hizi kwa uwazi zaidi na utazipata katika vitabu vifuatavyo:

1.   

AL-KAAFI

2.   

AL-BIHAAR

3.   

BASWAIRU-ADDARAJAAT

4.   

WASAAILU-SHIA

 

Hakika sisi tumefupisha habari hizi kwa kuwaleteeni riwaya moja kwa ajili ya  kufupisha.

Mimi  mpaka leo sifahamu wala sina uhakika iwapo kitabu hiki (AL-JAAMIA) kina ukweli wowote ule ama vipi jambo hilo bado limo nje ya fahamu zangu.na sijui kama ni kweli kwamba kitabu hicho kuna kila kitu  ambacho wanakihitaji watu mpaka siku ya Qimaya?ikiwa ni kweli basi ni kwa mimi kimefishwa? Na tukanyimwa sisi tusikipate ni hali ya kuwa kitabu hicho kimebainisha kila  jambo la halali na haramu pamoja na hukumu zote mpaka siku ya Qiyama,Je huku sikuficha elimu?hali ya kuwa kuficha elimu ni mambo yaliyo katazwa.Je kufanya hivyo sikatika kuficha elimu?jambo ambalo ni kinyume cha dini?!

 

2. SAHIFA YA AN-NAMUUSI.

Imepokewa kutoka kwa AL-RIDHAA (Alayhis Salaam) katika hadithi inayosimulia alama za imamu.Alisema-na Sahifa itakayo kuwa kwa imamu atakua na majina ya kishia(wafuasi) wao wote mpaka siku ya kiama.Na sahifa hiyo hiyo itakuwa imeandikwa na majina ya maadui zao wote mpaka siku ya kiyama.

Kwa ufafanuzi zaidi angalia:

1.   

BIHAAR AL AN-WAAR     Juzuu-25  Uk.117

2.   

BIHAAR AL AN-WAAR     Juzuu-26  Uk.117

Na utakuta riwaya nyingi zaidi.

 

Na mimi nikawa najiuliza uliza, ni kitabu cha aina  gani hicho ambacho kinaweza  kuandikwa majina   ya mashia wote mpaka siku ya kiyama!!!!. Na lau tungeweza kuya sajili majina ya washia wa IRAQ peke yake basi ingetulazimu kuhitaji  volume mia moja kwa uchache.na ingekuaje kama  tungesajili majina  ya mashia  wa IRAN na BARA HINDI na mashia wa PAKISTAN, SYRIA na LEBANON na DOLA ZA BARA  ARABU na nchi nyinginezo? Bali tungelihitaji  mijalada mengi kama tungesajili majina  ya watu waliokuisha kufa karne kwa karne zilizopita mpaka kudhihiri (kujitokeza) ushia mpaka zama hizi (wakati huu).

Na tungalihitaji vitabu vingapi vya kusajili majina ya mashia wetu katika karne zijazo mpaka siku ya kiyama? na tungalihitaji  vitabu vingapi vya kusajili majina ya mahasimu wao kuanzia kudhihiri hiyo sahifa AN-NAMUUS hadi siku ya Qiyama. Lau hata kama bahari ingalikuwa ni wino wa kuandikia  majina hayo na nyuma yake kukawa kuna bahari nyingine saba,basi wino wa bahari hizo usingeweza kutosha kuandikia majina hayo.

Na hatakama tungeweza kuzikusanya Computer zote za duniani pamoja na akili zote za ELECTRONI za kisasa vyote hivyo visingeweza kuhifadhi na kudhibiti majina hayo kutokana na wingi wake. Hata wale wajinga wasiokuwa na elimu,Akili zao haziwezi kukubali riwaya hizi (habari hizi) na mfano wake iweje watu wenye elimu na akili  timamu wawe wajinga kiasi hiki?!

Hakika ni  muhali mno na jambo lisilowezekana kwa maimamu  watukufu kusema mfano wa maneno haya ya  kipuuzi na  uwenda wazimu,kwani jambo hili halikubaliki kiakili na kimantik. Na lau kama maaduii zetu wangeweza kugundua riwaya hii  wangesema  wanavyotaka  juu ya  Uislamu wangeitusi dini ya kiislamu.na wangeweza kuusingizia Uislamu wanavyopenda.

 

 

3. SAHIFA YA AL-UBAYTAN

Imepokewa  kutoka kwa Amir-al muuminin (Alayhis Salaam) amesema,Ninaapa kwa jina la Allah, hakika mimi ninazo sahifa nyingi ambazo zimetoka kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).na kuna ndani ya sahifa hizo,sahifa inayoitwa (AL-UBAYTAN) na sahifa hiyo ina habari mbaya sana zinazo husu waarabu. Na mna habari za makabila  sitini ya kiarabu ambayo yameangamizwa wala hayana fungu lolote katika dini (yaani ni makafiri) Angalia  BIHAAR AL ANWAR- Juzuu 26  Uk.27.

Hakika riwaya hizi  hazikubaliki wala haziingii akilini, iwapo idadi yote hii ya makabila  itakuwa haina chembe ya dini mbele ya Allah,kwa maana hiyo ni kwamba hakupatikana hata muislamu mmoja ambaye atakuwa ana dini mbele ya Allah. Halafu kuhusisha haya makabila  kiaarabu kwa  hukumu hii mbaya hapa inapatikana harufu ya  ubaguzi wa kitaifa. Na  ufafanuzi zaidi utakuja katika mlango unaokuja

 

 

4. SAHIFA YA DHUABA AL-SAAIF.

Imepokewa kutoka kwa Abi Buswaira kutoka kwa Abi Abdillah(Alayhis Salaam),anasema kwamba kulikuwa kwa Dhuaba SAIF RASSULI kuna sahifa ndogo ndani ya sahfa hiyo kuna herufi nyingi na kila herufi moja katika herufi hizo hufunguliwa kwa herufi elfu moja.. na amesema Abu Buswaira , alisema Abu Abdillah na hazikutoka katika herufi hizo elfu moja ila herufi mbili tu,na itabaki hivyo hadi siku ya Qiyama. Angalia BIHARU AL- ANWAR Juzuu26 Uk: 56.

Mimi ni kasema na kujiuliza, na hizo herufi nyingine zilizobaki ziko wapi? Na kwa nini zisitolewe iliwafaidi mashia wa Ahlul Bayt?,kwa herufi hizo? Au zitabaki kuendelea kufichwa mpaka hapo atakapo simama AL QAIMU (Mahd).

 

 

 

5. SAHIFA YA ALI NAYO NI SAHIFA NYINGINE ILIYOPATIKANA KWA DHUABA AL-SEIFU.

Imepokewa kutoka kwa Abi Abdallah alisema ilipatikana kwa Dhuaba Saifu Rasul,sahifa ambayo imeandikwa ndani yake, BISMILLAHI RAHMAN RAHIM, hakika dhalimu mkubwa mbele ya Allah siku ya kiyama ni yule aliyeuwa asiyemuua, na yule aliyempiga asiye mpiga, na yule aliyetawala asiyestahiki kutawala.basi mtu huyo atakuwa ni kafiri aliye kufuru yale yote aliyoyateremsha Allah kwa Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). na mwenye kuzusha uzushi katika dini na yule aliyempa makazi kila mzushi mtu huyo, Allah hatamkubali siku ya kiyama kumkombolea hata fidia yoyote. Angalia BIHARU AL ANWAAR Juzuu 27  Uk: 65-104,na Uk: 275

 

 

6. AL-JAFAR: NA AL- JAFAR NI AINA MBILI:-JAFAR NYEUPE NA JAFAR NYEKUNDU.

Imepokewa kutoka kwa Abi Alaa alisema nilisikia Aba Abdillah (Alayhis Salaam) akisema hakika mimi ninayo AL-Jafar Nyeupe, na akasema Abi Aalaa kumuuliza Abi Abdillah, kwani mna nini ndani ya AL Jafar hiyo? Akasema Abi Abdillah: mna zaburi ya nabii Dauud mna Taurat ya nabii Musa na mna  injil ya nabii Issa na Suhfu ya nabii Ibrahim na mna upambanuzi kati ya mambo ya halali na haramu,na akaongeza kusema kwamba vilevile ninayo Al Jafar Nyekundu,na akaniuliza na mna nini  ndani ya Jafar Nyekundu akasema na kumjibu kwamba ndani yake mna silaha,na silaha hiyo ni mtu mwenye upanga kwa ajili ya kuuwa,na akasema Abdillah Bin Abii Yaafuur kumwambia Abi Abdilah kumwambia  kwa kumuombea dua;Allah akuweke katika afya njema. Je haya watakuwa wanayajua Banuu Al Hssan(kizazi cha Al Hassan) akamjibu ee!! Ndio wallahi wanayajua haya kama wanavyoujua usiku kwamba ni usiku na mchana kwamba ni mchana lakini wao wamepatwa na hasadi na kuitafuta dunia kwa kukanusha na kupinga haki, lau kama wangekua wanaitafuta haki kwa haki hilo lingekuwa bora kwao. Angaliaa USUULU AL KAAFI Juzuu 1 Uk: 24

Nilimuuliza maulana imamu Al Khui ambaye sasa ni aliyefariki, kuhusu Al jafar Nyekundu ni nani atakayeifungua? Na ni damu ya nani itakayomwagwa?.akanijibu na kusema kwamba atakayeifungua ni huyu bwana wa zama (Mwenyezi Mungu amfanyie haraka faraja yake)na watakao mwaga damu hiyo ni Ahlus Sunnah,kwa maana kwamba  watakuja kuuliwa  Ahlul Sunnat wote kwa pamoja na huyo  bwana wa wakati huo,na ataitawanya  damu yao na itakuwa nyingi sana na itakuwa inatiririka na kupita mto Dajital na Furat iliyoko IRAQ.

Na vilevile atakuja kulipizia kisasi kwa masanamu wawili wa kiquraysh (anakusudia maswahaba wa Mtume ambao ni makhalifa waongofu naye ni Abu Bakr na ‘Umar pamoja na Aisha Bint Abi Bakr na Bi Hafsa Bint ‘Umar ambao ni wake zake Mtume, pamoja na ‘Uthmaan Bin ‘Affaan ambaye ni mkwe wake Mtume pamoja na Bani Umaya na Bani Abbas.na hatimaye atakwenda kuyafukua makaburi yao na kuyawacha wazi.

Nikasema hakika kauli ya Imamu Al-Khui ni chafu na inachukiza mno,kwani Ahlul Bayt ni watu watukufu na wenye heshima kwani haiwezekani kwao kwenda kufukua makaburi ya maiti waliokufa kwa karne nyingi zilizopita(kwani watapata faida gani kwa hatua kama hiyo?). hakika maimamu (Alayhis Salaam) walikuwa wakiyakabili maovu  kwa kumtendea mema,muovu huyo na kumsamehe na kuyapuuza maovu yake.

Kw ahiyo haingii akilini kwa maimamu wenye sifa kama hii kuweza kuyafukua makaburi na kuwatoa hao maiti ili waweze kuwaadhibu na kulipizia kisasi na kuwasimamishia hadi (kuwahukumu)kwani maiti hawasimamishiwi hadi (kuhukumiwa hapa duniani) kwani Ahlul Bayt wote wanajulikana kwa sifa za usamehevu na kwamba ni watu wazuri wenye roho nzuri,kwani wao walikuwa ni watu wenye tabia njema walikuwa wavumilivu walibarikiwa tabia nzuri na hiyo ni nguzo madhubuti kabisa.

 

 

7. MAS-HAFU YA FAATIMAH

  1. Imepokelewa kutoka kwa Ali Bin said kutoka kwa Abi Abdilah,alisema: wallah tunao msahafu  wa FAATIMAH ambao una sura zote za kitabu cha Allah na msahafu huo ni maneno aliyoyasema Mtume na Ali akayaandika kwa mkono  wake. Tazama, BIHAAR AL ANWAAR. Juzuu 26 Uk: 41.

 

  1. Imepokewa kutoka kwa Muhammad ibn Muslim kutoka kwa mmoja kati ya hao maimamu wawili.Bi Ftma aliacha msahafu siyo Qur-ani kama tuliyokuwa nayo,lakini msahafu huo ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo aliyomteremshia Bi Fatmat khaswa , na mtu akasema maneno haya na Ali akayaandika  kwa mkono wake.  Tazama: BIHAARU AL ANWAAR Juzuu 26 Uk: 42.

 

  1. Imepokewa kutoka kwa Ali Bin Abii Hamza kutoka kwa  Abii Abdillah (Alayhis Salaam) alisema kwamba,sisi tunao msahafu wa Fatma, ama wallah ndani ya msahafu  huo hamna hata herufi moja ya Qur-ani, lakini msahafu huo ni maneno ya Mtume aliyo yatamka kisha akayandika kwa mkono wake. Angalia  AL BIHAAR  Juzuu 20  Uk:48.

 

Kisha nikasema na kujiuliza,ikiwa hiki kitabu ni maneno yanayotoka kwa Mtume na akayaandika Ali ni kwa nini basi akifiche kitabu hicho kwa Ummati wake kwani Mwenyezi Mungu akimuamrisha Mtume wake afikishe kila kitu alichoteremshiwa na Allah kwa Ummati wake kwani amesema Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat Al-Maaida: Aya; 67.

Vipi inawezekana kwa Mtume wa Allah kuweza kuwaficha waislamu wote Qur-an hii, na vipi inawezekana kwa Amir Al muuminina na maimamu wote waliokuja baadae kuificha Qur-an hiyo kwa mashia(wafuasi) wao.hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.

 

 

8. TAURAT NA INJIL NA ZABUR

Imepokewa kutoka kwa Abi Abdillah (Alayhis Salaam) kwamba yeye alikuwa akisoma INJIL na TAURAT na ZABUR kwa lugha ya kiisoiraniah. Tazama AL HUJAJ MINAL KAAFI, Juzuu 1 Uk: 208. mlango unaoelezea kwamba maimamu wote wanavyo vitabu vilivyoteremshwa kutoka mbinguni na Allah, na hakika hao maimamu wanavijua vitabu hivyo vyote pamoja  na tofauti za lugha za vitabu hivyo kwa maana kwamba maimamu wao wanazijua lugha za vitabu hivyo.

 

 

9. AL-QUR-AN

Kuthibiti kwa Qur-an kwamba ni kitabu cha Allah kisicho na shaka ndani yake hakuhitaji  nasuu (ushahidi).lakini utaona vitabu wa wanavyuoni wetu na kauli za mujitahidina (wanavyuoni wakubwa)wote  vinaelezea kwamba Qur-an hii imebadilishwa na sivyo ilivyo. Na hiyo Qur-an ndicho kitabu peke yake kilicho kumbwa na mabadiliko kati ya vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka nbinguni na Allah.

 Na hakika hivyo Al-Muhadith Annuury Atwabrisiy alitunga kitabu kikubwa sana katika kuthibitisha kwamba Qur-an imebadilishwa na kitabu hicho kinaitwa Faslu Al Khitwaab Fii Ithbaat Tahriif kitab Rabi-Al-Arbaabi. Na alikusanya ndani ya kitabu hicho zaidi ya riwaya Alfu moja zinazozungumzia juu ya kubadilisha Qur-an na vilevile akakusanya kauli za mafukaa wote na maulamaa wa kishia katika kubainisha na kuweka wazi juu ya kubadilishwa Qur-an ambayo ipo kwa waislamu.

Kwani wanazouni wote wa kishia na mafukaha wao wote kuanzia waliotangulia mpaka leo hii wanaamini na kusema  kwamba hakika ya Qur-an iliyopo hivi sasa kwa waislamu imebadilishwa Haifa kuwa nayo kwani siyo hawaiamini kamwe. Na huu ni uongo wa dhahiri wa kishia.

 

Amesema  Sayid Hashimu Al Bahraaniy: mimi ninao ushahidi wa kutosha juu ya kauli ya kwamba kubadilishwa kwa Qur-an, na hayo ni baada ya kufuatilia habari hizi kwa undani kabisa,kwa  kiasi ambacho inawezekana kutoa hukumu kwamba msimamo huu na itikadi hii ni katika jambo la dharura na  la lazima katika madhehebu ya  kishia kuamini hivyo. Na hakika hilo ndilo dhumuni kubwa la kunyang’anywa ukhalifa Ahl Bayt ; zingatia!!. Angalia: MUQADIMAT AL-BURHAN. Mlango wa tano, Uk: 49.

Na amesema Al Sayyid Niimatu Allah Al-Jazaairy, akiwajibu wale wanaosema kwamba Qur-an haikubadilishwa. Hakika kukubali ,na kuamini kwamba Qur-an, upokewaji wake,watu wake , una daraja ya Tawatur (upokeaji uliosahihi).na ni wahyi uliotoka kwa Allah na kwamba  Qur-an yote aliteremka nayo Jibril  kwa  amri ya Allah kutoka mbinguni,basi jambo hili  linapelekea kuweza  kuzitupilia mbali habari  ambazo zina ukweli na uhakika zaidi.pamoja na kwamba  wenzetu Ahlul Sunnat wamekubaliana kwa pamoja juu  ya   kusihi jambo hili na kuliamini moja kwa moja.Angalia AL-ANWAR ANNUUMANIYA . (Juzuu .2- Uk: 357.)

Na kwa habari hizi amesema Abu Jaafar kama ilivyonukuliwa na Jabir, amesema hakuna mtu yoyote ambae aliyedai kwamba Qur-an ilikusanywa mtu muongo kabisa. Nahakuna yoyote aliyekusanya na kuihifadhi hiyo Qur-an kama ilivyoshushwa isipokua Ali Bin Abi Twalib na maimamu baada yake. Angalia AL HUJAJI MINA AL KAAF-(Juzuu 1 Uk: 26.)

Bila shaka hii ni uthibitisho wa wazi kabisa unaothibitisha kubadilishwa Qur-an ambayo wanyo waislamu hivi sasa. Na Qur-an ya kweli ni ile ambayo iko kwa Ali na maimamu waliomfuatia baada yake yeye mpaka ikamfikia, ikawa huyo (AL QAAIM).

Na kutokana na hali hiyo ndipo aliposema AL-Imam Al- Khaui katika wasia wake kwetu sisi wakati akiwa anakurubia kufa alisema:Shikamaneni na Qur-an hii (ambayo imebadilishwa) mpaka itakapo dhihiri Qur-an ya Fatmah. Na Qur-an ya Fatmah anayoikusudia huyu Imam, ni ule msahafu ambao alioukusanya Ali kama tulivyoeleza nyuma.

 

Hakika ni jambo la kushangaza na kuchukiza kwamba vitabu vyote hivyo vimeteremka kutoka kwa Allah halafu vitabu hivyo viwe  vimemhusu Amirl muumini na maimamu wake baada yake.na vitabu hivyo vikasalia ni vyenye kufichwa kwa umma,na hasa kwa shia wa Ahlul Bayt isipokua Qur-an ndogo ambayo watu waliweza kuongeza wanachoongeza na kupunguza wanachopunguza. Haya ni kutokana na maneno ya wazuoni wetu wakishia.

Cha kushangaza  ni kwamba iwapo vitabu hivi vyote ni kweli vimeteremka kutoka kwa Allah na Amirl muuminina kuwa amekusanya na kuhifadhi Qur-an hii,sasa ina maana gani  yeye Amirl muuminin  kuwafichia ummah. Na hali yakuwa huo umma unahaja sana na Qur-an hiyo ambayo imekusanya taratibu zote za maisha yao ya kila siku na mambo ya ibada zao iliwaweze kumuabudu Allah, kama inavyotakikana?!.

Na wanazuoni (mafuqahaa) wetu wengi wamelielezea jambo hili na kuliletea kwa kila hali kwa ajili ya kuwaogopea upinzani. Na ni wajibu wetu sisi kuuliza, Je inawezekana akawa amirul muuminin ambaye pia ni simba wa Banu Hashim kuwa muoga kiasi cha kushindwa kutetea jambo hili? Je anaweza kuficha habari zake na kuunyima ummah kwa ajili ya kuogopa wapinzani wake. La sivyo ninaapa kwa yule aliyeziinua mbingu pasi na nguzo. Haikuwa kwa Ibn Abi Twalib akimuogopa yoyote isipokuwa Allah peke yake. Na  pindi tunapouliza  atafanya nini  Amirl muuminin na maimamu watakao kuja baada yake kwa Zabur na Taurat na Injil mpaka iwafikie watu wote na halafu waisome vitabu vyote hivyo kwa  siri.

Na ikiwakuna nasi (hoja) zilizodai kwamba Amiril muuminin ni yeye peke yake aliyehifadhi Qur-an yote, na akavihifadhi vitabu vyote vya mbinguni na sahifu nyinginezo. Sasa kuna haja gani tena kuwa ni Zaburi, Taurat na Injil? Na hasa tunajua ya kwamba vitabu vyote hivyo vimefutwa kwa kuteremka Qur-an?

Hakika mimi ninaona kwamba kuna mikono ya watu wanaotumbukiza sumu mbaya katika Riwaya hizi,na  wakawasingizia maimamu watukufu uongo huu, (na utakuja uthibitisho wa habari hizi katika  mlango maalum)

Sisi sote tunajuwa ya kwamba uislamu hauna kitabu isipokuwa kimoja nacho ni Qur-an tukufu. Ama kuwa na mfano wa vitabu vingi jambo hili ni maalumu kwa mayahudi na manasara kama ilivyokuwa wazi kwenye vitabu vyao,ama kauli inayosema kwamba  Amirl muuminin amevihifadhi jamii ya vitabu vyote na kwamba vitabu vyote hivyo vinatoka kwa Allah,na kwamba vitabu vyote hivyo vimekusanya mambo yote ya kishia kauli hiyo ni batil,imeingizwa kwetu na baadhi ya mayahudi ambao walijipenyeza kwenye ushia.

 

 

Share