11-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Uzinduzi 3

 

Ulianza  ushindani  baina ya watukufu na mujtahidina kwa ajili ya kupata khumus, na kwa ajili  hii alianza kila mmoja  kati yao kupunguza kiasi kinachotakiwa kuchukuliwa kutoka watu mpaka  watu wawe wengi kwake kuliko mwezake, wakajiwekea njia  za kishetani, mtu mmoja  alikuja kwa Asayid Asaysataniy akasema  kumwambia :

Hakika haki ya khumus ninayo takiwa kutowa ni milioni tano .nami nataka  kutoa nusu ya kiwango hicho yani milioni mbili na nusu,akamwambia  Asayid Asistaniy: lete hiyo milioni mbili na nusu, akampa  Asistaniy akazipokea, kisha akamwambia  : nimekupa wewe - yaani syyid Asistaniy akampa yule bwana alieleta zile hela -   yule  mtu akaichukua kisha,  akasema Asistaniy: rejesha tena kwangu hizo hela  yule mtu akampa tena, Asistaniy akamwambia sasa imekua mkusanyiko wake milioni tano dhima yako imeishaondoka katika khumsi, mabwana wakubwa wengine walipoyaona hayo wakafanya hivyo hivyo bali  wakavumbua njia nyingine,ili watu waende kutowa khumsi kwao na yakawa ni mashindano kati ya mabwana wakubwa kwa ajili ya kupata khumsi , na ikawa kiwango cha khumus kinafanana na biashara ya kupunguziana ,matajiri wengi wakawa wanaitowa khumsi kwa anae chukua kiasi kidogo .

 

Na mkuu wa chuo cha Najaf alipoona kuwa mashindano yamekuwa makubwa  na  kiwango kinacho ingia kwake ni kidogo, alitowa fatwa yake inayokataza kupewa khumsi mtu yoyote kati ya  watukufu, bali haitolewi isipokua  kwa watu maalumu, nae anafungu kubwa au mawakala wake alio wasambaza maeneo mbalimbali.

 

Na baada ya kuzipokea  mali hizi akawa anazibadilisha  kwa dhahabu kwa sababu ya hali duni ya hela ya iraki wakati huo , kiasi ambacho sasa hivi anamiliki vyumba viwili vya dhahabu .Ama kuhusu kiasi wanacho tumia mawakala wake sema utakavyo .

Amesema Amirul muuminin (Alayhis Salaam) wema ulioje kwa wenye kujitenga na dunia  na wakiwa na raghba ya akhera, basi hao ndio walioifanya ardhi vitanda na mchanga wake kuwa ni godoro na maji yake kuwa ndio manukato na Qur-aan ni alama yao , na  dua ndio nguo yao, kisha  wakaikopa dunia  kwa mfumo wa   masihi……. Hakika Daudi (Alayhis Salaam) alisimama  mfano wa saa hii ya usiku , na akasema hakika  ya saa hiii  hatoomba mja  isipokua hujibiwa , isipokuwa awe  Ahara u ayfa au Shartiya .[ Nahjul Balagha 4/24]  hebu linganisha kati ya maneno ya  Amirilul muuminin na hali za watukufu wa kishia na hukumu wewe mwenyewe , hakika  maelezo haya na mengineyo ni katika maelezo matukufu ambayo hayana kasoro yoyote mbele ya mabwana wakubwa na wanazuoni wa kishia ,  lakini  maisha ya fahari na raha na yafahari ambayo wanayaishi  yamewasahaulisha juhudi ya amiril-mumini na yakawafanya vipofu wasiweze  kuzingatia maneno yake na kushikamana na  maana ya maneno hayo.

 

Hakika asshar ni yule anayechukua kodi ya sehemu ya kumi katika mali, huyu dua yake  haipokelewi kama  alivyosema(Alayhis Salaam) basi itakuaje kwa mtu anaechukuwa  khumus? Ambae anaechukua khumus kwa watu? Hakika anae chukuwa khumsi anasababu ya msingi ya kutokubaliwa duwa yake, kwa sababu anacho kichuwa yeye ni zaidi ya kile anacho chukwa mtoza kodi . tunamuomba Mwenyezi Mungu afya.

Share