Mgonjwa Anaambiwa Ana Mashaytwaan Akivaa Pete Hutulia; Je, Avae Pete Au Itakuwa Ushirikina?

SWALI:

ASSALAMU ALAYKUM:

Kwanza natowa shukurani zangu kwa neema nyingi hizi mnazotupatia hapa Mwenyezimungu Awajalieni kila la kheri inshaallah.

Suali langu ni hili: Kuna mtu ana matatizo mengi tu yaani maradhi haya na haya yanajitokeza anakwenda hospital anafanyiwa uchunguzi na kupewa madawa na kutowa pesa kwa ajili ya matibabu Sasa huyu mtu ana jini sijui ndo shetwani kichwani mwake anakuwa anapanda kichwani na kusema mshaenda kuzitowa pesa zenu basi huyu ni mkaidi hanijali mimi kwani hatuoni sisi tumetajwa hata kwenye quran ananidharau sasa tatizo kuna pete fulani anataka aivae hiyo akiivaa tu maradhi yote yanapowa. Sasa huyu mama hataki kuivaa kwa sababu anaona akiivaa atakuwa anamuabudu yeye huyu shwaitwan. Sasa naomba mtusaidie kwa majibu yenu akiivaa hii pete kama ni kinga kwake itakuwa inafaa? Na hatokuwa yeye mushrik? Ahsanteni Ndugu yenu katika Imani


 

JIBU:

AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu mgonjwa kutulia kwa kuvaa pete fulani.

Kama mwanamke mwenyewe ambaye ni mgonjwa alivyofahamu ushirikina wa kuivaa hiyo pete ndivyo hivyo. Kwa kufanya hivyo mgonjwa atakuwa amemtii jinni au shaytwaani na Muislamu anafaa amtii Allaah Aliyetukuka tu.

 

Dawa ya mgonjwa huyu ni kusomewa Ruqyah ya Qur-aan na Shaykh mjuzi kwa hilo ambaye pia ni mchaji Mngu. Kwa kufanya hivyo huyo jini kama yuko kweli atatolewa na mgonjwa kutulia.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share