Kuomba Nguvu Kutokana Na Mizimu

 

Kuomba Nguvu Kutokana Na Mizimu  

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

A.a mashekhe alhamdullilah kwa kupata hii website ya kiislamu kwa kiswahili Allaah awazidishie imani. SWALI langu ni kuwa je yafaa kuomba mizimu kwa sababu kuna hata mashekhe fulani huenda kwa mizimu kuomba nguvu kutoka kwa mababu zao.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika ni maarufu kuwa mwenye kuombwa ni Allaah Aliyetukuka pekee. Ikiwa mtu atamuomba mwengine yeyote hiyo itakuwa ni shirki tena kubwa yenye kumtoa mtu katika Uislamu.

 

Allaah Aliyetukuka Anasema:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5].

 

Hivyo, wa kuombwa na Allaah Aliyetukuka peke Yake. 

 

Kwa hiyo, suala la kuomba mizimu haifai katika shari’ah yetu ya Kiislamu hata ikiwa inafanywa na anayejiita au kujidai ni shekhe.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share