Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Kwa Kamba Na Mboga Mchanganyiko

Chow Mein  (Tambi Nene Za Kukaanga)  Kwa Kamba Na Mboga  Mchanganyiko

 

Vipimo

Noodles (Tambi nene  za tayari) - 1 paketi

Mafuta ya ufuta (Sesame oil) - 3 vijiko vya supu

Kamba wakubwa (Prawns) - 2 LB

Nafaka mchanganyiko za barafu - 1 kikombe

Kabeji - ¼

sosi ya hardali (mustard) - 1 kijiko cha supu

Sosi ya soya (soy sauce) - 3 vijiko vya supu

Tomato ketchup - 2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilokunwa (grated) - 5 - 7 chembe

Tangawizi mbichi ilokunwa (grated) - 1 kipande

Paprika au pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Stock (kidonge cha supu) - 1

Maji ya moto - ½ kikombe

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

    

  1. Chambua noodles (tambi nene). Ikiwa ni zilozongoreka zikatekate kama kwenye picha.
  2. Chemsha maji na zipike kama inavyoelezwa katika paketi. Au chemsha kiasi ya dakika chache tu zisiive sana hadi zikawa laini sana. Chuja maji. Changanya na siagi ili zisigandane.
  3. Katakata kabeji vipande vya kiasi kwa urefu (grate) weka kando.
  4. Weka karai katika moto. Tia mafuta.
  5. Tia thomu na tangawizi mbichi ilokatwakatwa, kaanga kidogo kisha haraka tia  sosi zote,  tomato ketchup, paprika/pilipili nyekundu ya unga, chumvi endelea kukaanga kidogo.
  6. Tia kamba (prawns waliosafishwa na kumenywa maganda) endelea kukaanga waive.
  7. Tia nafaka mchanganyiko za barafu (frozen mixed peas) , changanya vizuri.
  8. Weka kidonge cha supu (stock) katika kibakuli na tia maji ya moto ½ kikombe na uikoroge ivurugike iwe supu.
  9. Mimina katika karai na changanya vizuri na mchanganyiko wa kamba. Acha muda wa dakika moja tu,  kisha epua katika moto.
  10. Kabla ya kupoa, tia kabejii na noodles/tambi  na changanya vizuri pamoja vyote. Weka katika chombo cha kupakulia ikiwa tayari.

 

Kidokezo:

  1. Sio lazima kupatikana tambi za aina hiyo ya paketi. Muhimu ni tambi zozote nene (noodles)
  2. Unaweza kutumia kitoweo kingine badala ya prawns.
  3. Ikiwa hukupata nafaka za barafu, tumia za kawaida ila ziache ziive zaidi katika mchanganyiko.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share