Majina Ya Watu Waliojitangazia Utume Kabla Na Baada Ya Kufariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

SWALI:

 

Swali. Napeda kujua majina ya watu walio Jitangazia Utume Kabla na Baada ya Kifo cha Mtume wetu (Amani ya mungu iwe juu yake) na nani aliye wauwa au kama walitubia.


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu majina ya waliojitangaza utume kabla na baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Wale waliojidai ni mitume katika zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni Musaylamah bin al-Habiyb al-Kadh-dhaab na Twulayhah al-Asadiy.

 

Ama wale waliojidai kuwa ni mitume baada ya kuaga dunia kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yaani wakati wa Ukhalifah wa Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakiwa ni al-Aswad al-‘Ansi na Sajaah bint al-Haarith bin Su’ayd.

 

 

Na baada ya hapo wapo waliojidai kuwa wanapata utume katika miaka ya baada ya hapo na mpaka wakati wetu huu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share