02-Swabrun Jamiyl: Fadhila Za Subra Katika Qur-aan

 

Swabrun Jamiyl (Subira Njema)

 

 

02-Fadhila Za Subra Katika Qur-aan

 

 

 

Subira imetajwa katika Qur-aan mara nyingi mno kama walivyonukuu ‘Ulamaa. Wengine wamesema kwamba imetajwa zaidi ya mara themanini kwa kusifiwa wale wenye kuvumilia mitihani inayowasibu. Ama kwa ujumla, subira imetajwa katika Qur-aan zaidi ya mara mia.

 

 

Zifuatazo ni baadhi ya fadhila za subira katika Qur-aan:

 

 

1.  Wenye kusubiri hupata mapenzi ya Allaah:

وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾

Na Allaah Anapenda wanaosubiri. [Aal-‘Imraan: 146]

 

 

2.  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yu pamoja nao daima:

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٤٦﴾

Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri. [Al-Anfaal: 46]

 

 

3. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Amewajumuishia mambo matatu ya bishara njema; Baraka (na maghfirah), rahmah Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na uongofu.

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾

 

Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

 

Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka. [Al-Baqarah: 155-157]

 

 

4. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi kuwalipa malipo mazuri kabisa kwa sababu ya kusubiri kwao katika utiifu.

 

 وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾

Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl: 96]

 

 

 

5. Wenye kusubiri wameahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  malipo mema yasiyohesabika.

 

  إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿١٠﴾

Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]

 

 

6. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameambatanisha subira na mafanikio na Amewaahidi kufuzu.

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu. [Aal-‘Imraan: 200]

 

إِنِّي جَزَيْتُهُمُ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿١١١﴾

Hakika Mimi Nimewalipa leo (Jannah) kwa yale waliyokuwa wakisubiri; hakika wao ndio wenye kufuzu. [Al-Muuminuwn: 111]

 

 

7. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewasifu kuwa ni miongoni mwa wakweli waliosadikisha na wenye taqwa.

 

وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾  

na wanaosubiri katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa. [Al-Baqarah: 177].

 

 

 

8. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi maghfirah na ujira mkubwa kwa wenye kusubiri na wakatenda mema.

 

إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١١﴾

Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema hao watapata maghfirah na ujira mkubwa. [Huwd: 11]

 

 

 

9. Wanaovumilia wamehusishwa na uongozi wa Dini na kuwa ni wenye yakini kuhusu yaliyoteremshwa kwao na Rabb wao.

 

 وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ ﴿٢٤﴾

Na Tukawajaalia miongoni mwao Maimamu wanaongoza kwa amri Yetu waliposubiri; na walikuwa wakiziyakinisha Aayaat (ishara) Zetu. [As-Sajdah: 24]

 

 

10. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Ameifanya subira kuwa ni kinga kubwa kwa maadui na hila zao kama walivyoaahidiwa Maswahaba katika vita vya Uhud.

 

 وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾

((Na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao. Hakika Allaah ni Mwenye kuyazunguka wayatendayo. [Aal-‘Imraan: 120]

 

 

 

11. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Ameifanya kuwa ni jambo la kutakwa msaada pamoja na nguzo ya Swalaah na kuwasifu kuwa wenye kuvumilia ni wenye sifa ya unyenyekevu.

 

 وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu. [Al-Baqarah: 45]

 

 

 

12. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewasifu wenye kuvumilia misiba, maudhi na dhulma kwamba hilo ni jambo kuu la kuazimiwa.

 

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [Ash-Shuwraa: 43]

 

 

 

13.  Wenye kuvumilia bila shaka watapewa kheri nyingi na wenye hadhi kubwa.

 

 وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾

Na hapewi hayo isipokuwa wale waliovuta subira, na hapewi hayo isipokuwa mwenye fungu adhimu. [Fusswilat: 35]

 

 

 

14. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Ameambatanisha ushindi kwa subira na taqwa.

 

بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴿١٢٥﴾ 

Bali, ndio! Mkisubiri mkawa na taqwa na wakakujieni kwa ghafla hivi (kukutekeni); Rabb wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tano waliotiwa alama ya ubora. [Aal-‘Imraan: 125]

 

 

 

15. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesifu kila ambaye ananufaika na Aayah Zake na akaathirika na mawaidha kwamba ni mwingi wa kusubiri na kushukuru:

 

 إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٣٣﴾

Hakika katika hayo mna Aayaat (zingatio, ishara) kwa kila mwingi wa kuvuta subira na mwingi wa kushukuru. [Ash-Shuwraa: 33]

 

 

16.  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemsifu Nabiy Ayyuwb (‘Alayhis Salaam) kwa subira yake kuwa ni mja mzuri alioje.

 

 إِنَّا وَجَدْنَاهُ صَابِرًا ۚ نِّعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٤٤﴾

Hakika sisi Tulimkuta mwenye subira mno, uzuri ulioje wa mja, hakika yeye ni mwingi wa kurudiarudia kutubia. [Swaad: 44]

 

 

 

17.  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amehukumu kukhasirika kwa mwana Aadam pindi asipokuwa miongoni mwa wenye kuusia subira na akavumilia  mwenyewe pia:  

 

وَالْعَصْرِ ﴿١﴾

Naapa kwa Al-‘Aswr (zama).

إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾

Hakika mwana wa Aadam bila shaka yumo katika khasara.

 

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana haki na wakausiana subira. [Suratul-‘Aswr]

 

 

18. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Amewahusisha watu wa kuliani ambao ni watu wa kheri kwamba ni watu wenye subira wenye huruma.

 

 ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾

Kisha akawa miongoni mwa wale walioamini, na wakausiana kusubiri na wakausiana huruma.

 

أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾

Hao ndio watu wa kuliani. [Al-Balad: 17-18]

 

 

 

19. Hatimaye huko Aakhirah ambako ndio kwenye maisha ya kudumu na milele wameahidiwa Jannah na Neema zake:

 

 وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا﴿١٢﴾

Na Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Jannah na nguo za hariri. [Al-Insaan: 12]

 

 

 

20.  Na pia watabashiriwa Jannah na neema zake na amani kutoka kwa Malaika.

 

 جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ﴿٢٣﴾

Jannaat za kudumu milele wataingia pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao na wake zao na dhuria zao. Na Malaika wanawaingilia katika kila milango.

 

سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ ۚ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٤﴾

 “Salaamun ‘Alaykum! (Amani iwe juu yenu) kwa yale mliyosubiri.” Basi uzuri ulioje hatima njema ya makazi ya Aakhirah. [Ar-Ra’d: 23-24]

 

 

Lakini si wepesi kuipata Jannah, na miongoni mwa watakaiopata ni wale waja waliosubiri katika kufanya jihaad katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wakakumbwa na mitihani na mateso mbali mbali. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Amewatia mtihanini ili Awatambue kama walivumilia kweli:

 

 أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٢﴾

 

Je, Mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali Allaah Hakudhihirisha wale waliofanya jihaad miongoni mwenu na Akadhihirisha wenye kusubiri? [Aal-‘Imraan: 142]

Share