Wanawake Kufanya Muhadhara Na Kuimba Kaswida Katika Sherehe Za Ndoa

SWALI:

 

ASSALAM ALEIKUM WARHMATULLAH WABARAKATUH. NDUGU ZANGU WA ALHIDAAYA, SWALI NI HILI AMBALO LINALETA UTATA, IKIWA BAADHI YA MASHEKH WANASEMA, MUHADHARA WAKUMFANYIYA BINTI AMBAYE ANATAKA KUFUNGA NDOWA NI MAKOSA, IKIWA MWENYEZIMUNGU ANASEMA FICHA UCHUMBA UTANGAZIYE NDOWA, SASA IKIWA UTAFANYA MUHADHARA WA KINA MAMA PEKE YAWO MFURAHIYE PAMOJA NA MUIMBE KASWIDA NA NASAHA ZA NDOWA MUMFIKISHEYE BI HARUSI, JE KUNA MAKOSA KUHUSU HUYO MUHADHARA WAKIDINI WAKUNDI LAKINA MAMA? NA KAMA NIMAKOSA TULIKUWA TUNAOMBA MTUFAHAMISHE NILIPI KOSA? NA MTUFAHAMISHE NI LIPI LAKUWEZA KULIFANYA IKIWA BINTI ANATARAJI KUFUNGA NDOWA. WAHADHA ASSALAM ALEIKUM WARHMATULLAH WABARAKATUH. TUNASUBIRI MAJIBU INSHAALLAH.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kufanya muhadhara wa ndoa na kuimba kaswida wanawake wao peke yao.

 

Mtume wetu karuhusu wanawake kuimba na kupiga dufu katika minasaba miwili; siku ya ‘Iyd na siku ya harusi.

 

Ama kuhusu muhadhara hakika hiyo ni fursa nzuri ya furaha ya kuwakumbusha wanawake kuhusiana na wajibu wao wa Kidini na pia kutekeleza malezi mema kwa kizazi kijacho. Hivyo, hapana ubaya wowote wa kufanya mhadhara na kukumbushana masuala mbalimbali likiwemo hilo la nasaha za ndoa.

 

Ama kuhusu kusherehekea ndoa na kuimba Qaswiyda, hakika ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anahimiza kukiwa na harusi basi wanawake wawe ni wenye kuimba kama alivyomwambia mkewe Aa’ishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kuhusiana na hilo.

Kwa hiyo, mnaweza kufanya mhadhara na kuelimishana masuala ya ndoa. Na mkasubiri siku ya ndoa yenyewe mkaimba Qaswiydah/Nashiyd kinamama na kupiga dufu na kufurahi kwa ajili ya ndoa hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share