Uhalali Kwa Mwanamme Kufanya DNA Test Ili Kuhakikisha Kuwa Mtoto Ni Wake

SWALI:

Je ni halali kwa mwanamme kufanya DNA test ili kutaka kujua kwamba mtoto kweli ni halali yako labda kwa kutaka kuondoa shaka?


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kufanya DNA test ili kuhakikisha kama mtoto ni wako kweli.

Ni ajabu kwa mwanamme kuanza kumshuku mkewe kuwa anatembea nje kwani kufanya hivyo kunavunja kabisa uhusiano wa kindoa na kukosa utulivu kwa kiroho na kimoyo. Mwanamme au mwanamke akianza tu kumshuku wapili wake katika ndoa ndio kuivunja ndoa yenyewe.

Ndoa ni mapenzi na kuhurumiana baina ya wanandoa. Na kupata natija hiyo ni lazima wanandoa wawe ni wenye kuaminiana kwa kiasi kikubwa kwani kutoaminiana ni wasiwasi unaoingiszwa na Shaytwaan na Shaytwaan ni adui mkubwa sana mwa mwanaadamu.

Kwa hiyo, ondoa shaka wala usiende kufanya DNA test kwa hali yoyote ile. Kuwa na imani na mkeo kuwa ni mwaminifu na Insha Allaah Allaah Aliyetukuka Atakuondoshea wasiwasi huo usio mzuri.

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:

Nini Hukmu Ya DNA Katika Uislam

Kuwatambulisha Watoto Bila DNA

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share