Ndoa Yenye Uhusiano Na Ndugu, Jamaa





SWALI

asalam alaykum.

Jamani kuna suali linanitatiza, kwa mfano, mimi na ndugu yangu wa baba mmoja mama mmoja tukazaa watoto, mtoto wangu akaja kupata mtoto na yeye ambaye mie itakuwa ni mjukuu wangu, je huyu mjukuu wangu naweza kumuoa mtoto wa kaka yangu ambaye ni haloo yake. Nataraji majibu mazurikutokwa kwenu.



Bottom of Form

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Shukran kwa swali lako zuri. Mara nyingi sisi kama Waislamu huteleza katika baadhi ya mambo kwa sababu huchanganya Dini yetu ambayo imekamilika na mila na desturi zetu za kifamilia au kikabila. Na katika suala hili la ndoa Uislamu una sheria yake ambayo inatakiwa ifuatwe na kila Muislamu. Wale wanawake ambao mwanamume hafai kuwaoa wapo wazi katika Qur-aan, hivyo wasiokuwa hao anaweza kuwaoa bila ya tatizo lolote. Je, hao wanawake ni wapi? Wao ni kama wafuatao:

    1. Mama zenu.

    2. Wanawake walio olewa na baba zenu (mama wa kambo).

    3. Binti zenu.

    4. Dada zenu (shaqiqi, kwa mama tu au kwa baba tu).

    5. Shangazi zenu.

    6. Halati zenu (mama mdogo).

    7. Binti wa kaka zenu.

    8. Binti wa dada zenu.

    9. Mama waliowanyonyesha.

    10. Dada zenu kwa kunyonya.

    11. Mama wa wake zenu.

12. Watoto wenu wa kambo (wazawa wa wake zenu kwa mume mwengine na ambao mumewaingilia).

    13. Wake wa watoto wenu (muliowazaa).

    14. Dada wawili kwa wakati mmoja.

    15. Na wanawake ambao wameolewa ( – 24).

Kulingana na swali, je, msichana ni miongoni mwa hawa waliokatazwa? Ikiwa yupo katika orodha hii ndoa itakuwa haifai na lau hayupo basi wanaweza kuowana.

Hebu tulitizame suala hilo kwa makini. Baba ana watoto wawili Mtoto A na Mtoto B, A akapata mtoto C na C akapata mtoto ambaye ni D. huyu B naye alipata mtoto ambaye ni E (wa kike). Kinasaba E anakuwa ni halati yake D, lakini kisheria wanaweza kuoana kwa sababu halati si kama mama mdogo kwani baba zao na mama zao ni tofauti. Mfano huo ni kama ile ndoa ya ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Faatwimah bint Rasuul (Radhiya Allaahu ‘anha), japokuwa ‘Aliy anakuwa ni ‘ammi yake kinasaba.

Kuelezea ndoa hiyo ni kuwa huyu baba wa juu ni ‘Abdul-Mutwallib ambaye alipata watoto A (‘Abdullaah) na B (Abu Twaalib). A alimzaa C (Mtume [Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam]), naye akamzaa bintiye D (Faatwimah). Na B naye alimzaa E ambaye ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu). Kinasaba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni ndugu (binamu) lakini kisheria mtoto wa mmoja anaweza kuolewa na mwenziwe.

Na Allah Anajua zaidi

 

Share