Saladi Ya Tabbulah 1 - Lebanon

Saladi Ya Tabbulah 1 - Lebanon

Vipimo na Namna ya Kutayarisha

Parsley (aina ya kotmiri) osha, chuja maji katakata (chop) - 4 misongo (bunches)

Nanaa (mint leaves) - 1 msongo

Vitungu majani (spring onions) katakata vidogodogo -  7

Kitunguu maji  - 2

Tungule nyanya ya kawaida - 3 kubwa

Matango – 3

Burghur (ngano ilokobolewa) Tazama picha - ¼  kikombe

Limau kamua - 2

Chumvi – kiasi

Mafuta ya zaytuni - 1/3 kikombe

Namna Ya Kutayarisha

1. Osha bulgur tia maji roweka muda robo saa, kisha ichuje maji na ukamue itoke maji yote.

 

2. Katika bakuli weka vitu vyote isipokuwa limau, chumvi na mafuta ya zaytuni.

3. Karibu na kupakua changanya bulgur, limau na mafuta ya zaytuni katika kibakuli kidogo kisha mwagia na changanya pamoja na vitu katika bakuli.

Kidokezo:

Hakikisha umechuja maji majani na vitu vyote kwani Tabbulah hulegea mara moja. Na pia ni vyema kuchanganya vitu karibu na wakati wa kupakua  

 

Share