Fadhila Za ‘Umrah Na Hajj - Kutoka Kitabu: Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah

 

Fadhila Za ‘Umrah Na Hajj 

Kutoka Kitabu: Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kuna fadhila nyingi zinazopatika kwa kutekeleza ‘ibaadah hizi tukufu. Muislamu anayetaka kuzipata fadhila hizo, lazima afuate amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:

 

 الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

((Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!)) [Al-Baqarah: 2: 1971]

 

Kadhaalika, kuna fadhila nyinginezo kadhaa ambazo Muislamu anafaidika nazo zinazohusu Dini na dunia yake: Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴿٢٨﴾

 ((Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo. Basi kuleni humo, na lisheni mwenye shida fakiri.))  [Al-Hajj  22: 28]

 

 

Aayah hii imetaja baadhi ya manufaa ya ki-Dini na ya kidunia. Ya ki-Dini ni kujichumia thawabu tele katika kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwenye masiku machache matukufu yaliyojaa fadhila adhimu. Ama manufaa ya kidunia yaliyotajwa humo ni mnyama wa kafara ambaye nyama yake inagaiwa kwa masikini. Manufaa mengineyo ni kama yafuatayo:

 

 

Manufaa Ya ki-Dini

 

 

1. Hajj Na ‘Umrah Ni Kupata Radhi za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

Hajj ina taathira kubwa katika moyo wa Muislamu. Humbakisha katika taqwa na iymaan ya hali ya juu. Kwa wengineo iymaan zao huwa nzuri zaidi na mabadiliko haya huwa ni ya kudumu katika uhai wao.

 

Hajj au ‘Umrah humjaza mapenzi Muumini moyoni mwake apende kurudia kutekeleza ‘ibaadah hizi tukufu. Hii ni kutokana na du’aa ya Nabiy Ibraahiym(عليه السلام)  baada ya kumaliza kujenga Al-Ka’bah alipoomba:

 

رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾

 ((“Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde (la Makkah) lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru)) [Ibrahiym: 14: 37] 

 

 

2. Hajj Na ‘Umrah Ni Kujichumia thawabu tele za kuswali katika Masjid Al-Haraam.

 

عَنْ جَابِرٍ )رضي الله عنه( أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ، وَصَلَاةٌ فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَفْضَلُ مِنْ مِائَةِ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ)) رواه أحمد وابن ماجه

Imepokelewa toka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Swalaah katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swalaah elfu kwengineko isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam. Na Swalaah katika Al-Masjid Al-Haraam ni bora kuliko Swalaah elfu mia (laki moja) kwengineko)) [Ahmad, Ibn Maajah]

 

 

3.  Hajj Ni Kufutiwa madhambi yote. 

               

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: "سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ حَجَّ لِلَّهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ)) متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah(رضي الله عنه)  kasema: “Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه  وآله وسلم) akisema: ((Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

  

 

4. Hajja Jazaa yake Jannah.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((العُمْرَةُ إِلَى العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا، وَالحَجُّ المَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلَّا الجَنَّةَ)) متفق عليه  

Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: (('Umrah hadi 'Umrah ni kufutiwa dhambi baina yao, na Al-Hajjul-Mabruwr haina jazaa isipokuwa ni Jannah)) [Al-Bukhaariy]

 

 

5.  Hajj Ni Katika ‘Amali bora kabisa:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) سُئِلَ: أَيُّ الْعَمَلِ أَفْضَلُ؟ فَقَالَ: ((إِيمَانٌ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ)) قِيلَ:  ثُمَّ مَاذَا؟ قَالَ: ((الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ)) قِيلَ:  ثُمَّ مَاذَا؟ قَالَ:  ((حَجٌّ مَبْرُورٌ)) متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba aliulizwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Ni ipi ‘amali iliyo bora zaidi?” Akasema: ((Kumuamini Allaah na Rasuli Wake)) Akaulizwa: "Kisha ipi"? Akasema: ((Jihaad katika Njia ya Allaah)) Akaulizwa: "Kisha ipi"? Aakasema: ((Hajjum-Mabruwr)) [Al-Bukhaariy, Muslim] 

 

6.   Hajj Ni Jihaad bora kabisa kwa wanawake.

 

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا)  قَالَتْ  قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَرَى الْجِهَادَ أَفْضَلَ الْعَمَلِ, أَفَلا نُجَاهِدُ مَعَكَ؟ قَالَ: ((لا وَلَكِنَّ أَفْضَلَ الْجِهَادِ حَجٌّ مَبْرُورٌ))

Kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: “Tulisema: Ee Rasuli wa Allaah, (kwa vile) tunaona jihaad kuwa ni ‘amali bora kabisa. Je tusifanye jihaad pamoja na wewe?” Akajibu: ((Hapana! Jihaad bora kabisa ni Hajjum-Mabruwr)) [Al-Bukhaariy]

 

7.  Hajj Inaondosha ufakiri na madhambi.

 

عَنْ ابْنُ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تَابِعُوا بَيْنَ الْحِجِّ وَالْعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الْفَقْرَ وَالذُّنُوبَ، كَمَا يَنْفِي الْكِيرُ خَبَثَ الْحَدِيدِ  والذهب والفضة وليس للحج المبرور ثواب دون الجنة)) رواه أحمد والترمذي وصححه، والنسائي وابن خزيمة في صحيحه صححه الشيخ الألباني رحمه الله في  السلسلة الصحيحة

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم) amesema: ((Fuatilieni Hajj na ‘Umrah kwani hizo [mbili] zinaondosha ufakiri na madhambi kama kinavyoondosha chombo cha kupulizia moto uchafu wa chuma na dhahabu na fedha, na Al-Hajjul-Mabruwr thawabu yake hakuna zaidi ya Jannah)) [Ahmad, At-Tirmidhiy na ameisahihisha, na An-Nasaaiy na ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Silsilat Asw-Swahiyhah]

 

8.  Kuwa ni mgeni wa Allaah (سبحانه وتعالى) na kutakabaliwa du’aa.

 

Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

((الْغَازِي فِي سَبِيلِ اللَّهِ، وَالْحَاجُّ، وَالْمُعْتَمِرُ، وَفْدُ اللَّهِ، دَعَاهُمْ فَأَجَابُوهُ، وَسَأَلُوهُ فَأَعْطَاهُمْ))  رواه ابن ماجه-واللفظ له-، وابن حبّان في "صحيحه"    

((Anayepigana jihaad katika njia ya Allaah, na anayefanya Hajj na ‘Umrah ni wageni wa Allaah, Amewaita wakamuitikia, wakamuomba Akawatakabalia)) [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika Swahiyh zao]  

 

9.  Kuhudhuria darsa katika Misikiti mitukufu kabisa na kukutana na Wanachuoni.

 

 

Manufaa Ya Kidunia

 

 

1-Kukutana na kujuana na Waislamu wengineo kutoka pande mbali mbali za dunia, kutambua hali zao, kuunganisha mawasiliano na kushirikiana nao kwa kheri.

 

2-Historia ya Uislamu na baadhi ya matukio katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

3-Kuliwazika na matembezi mbali mbali ya miji na yanayohusiana na safari kwa ujumla; mandhari za miji, kubadilisha hewa na chakula, kujinunulia mahitaji na zawadi.

 

4-Kufanya tijara kwani imeruhusiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema:

 

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ   

((Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu))  [Al-Baqarah 2: 198]

 

 

 

 

Share