Sha'baan: Uzushi Wa Mashia Wa Swalah Ya Usiku Wa Mwanzo Wa Sha'baan

 

Uzushi Wa Mashia Wa Swalaah Ya Usiku Wa Mwanzo Wa Sha'baan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalaam Aleikum

Nimetumiwa hii habar lakini haionyeshi inatokana na hadithi gani je hii ina uhakika.

 

hii ni sala unayosali  ucku wa kuingia shaaban ukijua tu mwezi umeandama usali rakaa12 sali rakaa  mbili mbili.nia.uswali rakaa tayn sunnat awal laylat min shaaban lillah taala allahu akbar.utasoma alhamdu na kulhuwallahu 15 kwa kila rakaa.  Faida yake allah atakupa thawabu za mashahid 10000 na utaandikiwa thawabu ya miaka 12 na hufutiwa madhambi kama unatoka katika tumbo la mama yako leo na hutoandokiwa dhambi kwa muda wa siku 80.allahu aalam allah atupe wepec inshaallah.warushie waislam wengine

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

 

Hiyo Swalaah inayodaiwa ya mwezi wa Sha’baan si sahihi bali ni uzushi wa Mashia.

 

Hakuna Swalaah ya aina hiyo wala hakuna Hadiyth yoyote katika vitabu vya Waislamu inayofundisha Swalaah hiyo.

 

 

Baada ya utafiti imegundulika ni uzushi wa Mashia uliopo katika kitabu chao kiitwacho Wasaail Ash-Shiy’ah.

 

 

Waislamu wanapaswa kujihadhari sana haswa masiku haya ambapo ujumbe unaenezwa kwa haraka kupita kiasi na makundi potofu yakilingania Uzushi wao.  ‘Ibaadah za Muislamu hazipokelewi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mpaka zitimize masharti mawili. 

 

1. Ikhlaasw  

2. Mutaaba'ah (kufuata mafunzo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  

 

 

Kwa hiyo, madamu hakuna dalili ya ‘Ibaadah hiyo inabakia kuwa ni uzushi na Muislamu anapaswa kujiweka mbali nao.

 

 

Tahadharini Waislamu kueneza uzushi kama huo na mwengine unaosambazwa kwa njia za mitandao ya kijamii na kumbi za kijamii.  

 

 

Kuna khatari kubwa katika kuzusha au kueneza uzushi na kumnasibishia nao Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyosema katika Hadiyth iliyopokelewa na 'Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw  (Radhwiya Allaahu 'anhumaa):

 

"Mwenye kunizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni". [Al-Bukhaariy]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share