Kuzini Ndani Ndoa Nini Hukmu Yake?
SWALI:
Assalaam alaykum.
Swali langu ni.
Naomba kuuliza kua mke akiwa amezini na akamtamkia mume wake kua amefanya hicho kitendo itakua ameachika kwa kufanya hicho kitendo au mpaka mume ampe talaka ndioa kaachika. Na pia itakua mke keshaharamika kwa mume wake? Au, naomba majibu inshaalla mapema ikiwezekana ameen
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa ndugu yetu kwa swali lako hili. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuepushe na magonjwa haya ya zinaa na maasiya mengineyo. Ieleweke kuwa mke ana madhambi kwa kitendo hicho chake cha kuzini. Kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakayefanya hayo atapata madhara, Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyaamah, na atadumu humo kwa kufedheheka” (25: 68 – 69).
Lau kama kungelikuweko Dola ya Kiislamu ambayo ingelitimiza adhabu ya kumpa mwenye kuzini, basi bila shaka maasi haya yangeliogopewa na kila Muislamu. Hivyo bila shaka hakuna yeyote ambaye angelithubutu kufanya maasi haya.
Hivyo ingelibidi kwa kukiri kwake kuwa kazini, hukumu yake ingekuwa ni kuuliwa
Mke kama huyu bado hajaachika mpaka mume wake ampatie talaka.
Mke huyo bado ni mke wa mtu na ikiwa mume atamsamehe kwa kule kutaka msamaha kwake basi ndoa
“Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Allaah, Mola wenu Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Allaah, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Allaah, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Allaah ataleta jambo jengine baada ya haya” (65: 1).
Maelezo ya maana ya Aayah hii
Surah hii inataja habari nyingi zilizokhusiana na talaka. Talaka kama alivyosema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) dhahiri shahiri katika Hadithi zake.
Talaka imewekwa itokee itakapotokea dharura iwe
Basi hapa zinatajwa kidogo sharti za kuacha:
i) Fatwalliquu-hunna li'ddatihinna
Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifasiri tamko hili kwa kuwa hapana ruhusa kumuacha mwanamke anapokuwa yumo:
a) Miezini au
b) Katika tahara lakini wampeta kuonana katika tahara hiyo.
Mwanamume akipandwa na hamaki akataka kumuacha mkewe hana ruhusu kumuambia: "Nimekuacha". Lazima amuulize kwanza yumo miezini (katika hedhi) au
Kama yuko miezini, basi itampasa angojee mpaka aingie katika tahara ndipo amuache. Na Wakati huo hawataachana tena kwani shetani atakuwa kisha kuruka zamani.
Na ikiwa yumo katika tahara waliyoingiliana, basi lazima angojee mpaka tahara hiyo ishe, aingie miezini, ishe ada yake ya mwezi aingie katika tahara. Kabla ya kuingiliana amuache. Wala hawataachana vile vile kwani shetani atakuwa ameruka zamani.
ii) Laa tukhrijuuhunna min buyuutihinna
Msiwatoe katika majumba
Mume ndiye ajitenge chumba mbali na choo mbali. Ikiwa hapana nafasi, basi atoke yeye mume akatafute nyumba nyingine ya kukaa mpaka ishe eda ndiyo bibi atokea na achukue vyake. Na wala hatawahi kutoka kwani pengine watakuwa wamekwisha kurejeana. Inataka awe shetani mkubwa huyo hata muda wa miezi mitatu kuwa bado tu hajawatoka! Basi hii ndio Laalla-Llaaha Yuhdithu Ba'ada Dhaalika Amra.
iii) Wa-ahswul-'iddah
Wadhibiti siku za eda ili warejeane kabla ya kumalizika.
Na Allah Anajua zaidi