Imaam Ibn Rajab - Kunasibishwa Mwezi Wa Al-Muharram Na Allaah

 

Kunasibishwa Mwezi Wa Al-Muharram Na Allaah 

 

Ibn Rajab (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu-Allaah) amesema:

 

"Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameuita mwezi Al-Muharram kuwa ni Mwezi wa Allaah na kuunasibisha kwa Allaah inaashiria utukufu na fadhila zake kwani Allaah hunasibisha kwake kile ambacho ni makhsusi miongoni mwa viumbe Vyake, mfano; Alivyomnasabisha Muhammad, Ibraahiym, Is-haaq, Ya’-quwb na wengineo miongoni mwa Manabii - kuwahusisha na 'ubuwdiyyah Yake. (Yaani  Amemwita Muhammad: “Mja Wake” [Suwrat Al-Israa: 1, An-Najm: 10],  Akawataja hao wengine kama ni: “Waja Wangu” [Suwrat Swaad: 45]) Akajinasibisha na Nyumba Yake (Yaani Al-Ka’bah kwa kusema “Nyumba Yangu” [Al-Baqarah: 125]) Na ngamia Wake wa kike (Yaani kusema: “Ngamia wa kike wa Allaah” [Suwrat Al-A’raaf: 73, Suwrat Ash-Shams: 13])

 

 

[Latwaaif Al-Ma’aarif, uk. 36]

 

Share