037 - Asw-Swaaffaat

 

  الصًّفَّات

 

037-Asw-Swaaffaat

 

 

 

037-Asw-Swaaffaat: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالصَّافَّاتِ صَفًّا ﴿١﴾

1. Naapa kwa (Malaika) wanaojipanga safusafu.

 

                                              

 

 

فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosukumiza mbali mawingu.

 

 

 

 

فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosoma Maneno ya Allaah.

 

 

 

 

إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ ﴿٤﴾

4. Hakika Mwabudiwa wenu wa haki bila shaka Ni Mmoja.

 

 

 

 

 

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ ﴿٥﴾

5. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na Rabb wa mapambazuko.

 

 

 

 

إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ ﴿٦﴾

6. Hakika Sisi Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mapambo ya nyota.[1]

 

 

 

 

 

وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ ﴿٧﴾

7. Na hifadhi kutokana na kila shaytwaan asi.

 

 

 

 

 

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ﴿٨﴾

8. Hawawezi kulisikiliza kundi la juu lililotukuzwa, kwani wanavurumishwa kila upande.

 

 

 

دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ ﴿٩﴾

9. Wakifukuziliwa mbali, na watapata adhabu ya kuendelea.

 

 

 

 

 

إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ﴿١٠﴾

10. Isipokuwa yule atakayenyakua kitu kwa kuiba, basi kitamwandama kimondo kiwakacho.

 

 

 

 

فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَا ۚ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍ ﴿١١﴾

11. Basi waulize: Je, wao ni viumbe wenye nguvu zaidi, au wale Tuliowaumba? Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na udongo unaonata.

 

 

 

 

بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ ﴿١٢﴾

12. Bali umestaajabu, nao wanafanya dhihaka.

 

 

 

 

وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ ﴿١٣﴾

13. Na wanapokumbushwa, hawakumbuki.

 

 

 

 

وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ ﴿١٤﴾

14. Na wanapoona Aayah (Ishara, Dalili) wanazidi kufanya dhihaka.

 

 

 

 

وَقَالُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Na wanasema: Haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.

 

 

 

 

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾

16. Je, hivi tukifa, na tukawa vumbi na mifupa, hivi sisi tutafufuliwa?[2]

 

 

 

 

 

أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿١٧﴾

17. Je, pia na baba zetu wa awali?

 

 

 

 

قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ ﴿١٨﴾

18. Sema: Naam (mtafufuliwa), hali na nyinyi ni madhalili.

 

 

 

فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ ﴿١٩﴾

19. Kwani huo ni mngurumo (wa baragumu) mmoja tu, tahamaki hao wanatazama!

 

 

 

وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿٢٠﴾

20. Na watasema: Ole wetu! Hii ni Siku ya Malipo.

 

 

 

 

هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢١﴾

21. (Wataambiwa): Hii ndio Siku ya hukumu ambayo mlikuwa mkiikadhibisha.

 

 

 

 

احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾

22. (Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu.

 

 

 

 

مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾

23. Badala ya Allaah. Basi waongozeni kwenye njia ya moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ ﴿٢٤﴾

24. Wasimamisheni. Hakika wao wataulizwa.

 

 

 

 

مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾

25. Mna nini hamnusuriani?

 

 

 

بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾

26. Bali wao leo wamesalimu amri.

 

 

 

 

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na watakabiliana wenyewe kwa wenyewe kuulizana.

 

 

 

 

قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ ﴿٢٨﴾

28. Watasema: Hakika nyinyi mlikuwa mkitujia kwa nguvu na ushawishi.

 

 

 

 

قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾

29. Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa wenye kuamini.

 

 

 

 

وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ ﴿٣٠﴾

30. Na hatukuwa na madaraka yoyote juu yenu, bali mlikuwa watu wapindukao mipaka kuasi.

 

 

 

 

فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ ﴿٣١﴾

31. Basi ikahakiki juu yetu Kauli ya Rabb wetu. Hakika sisi bila shaka tutaonja (adhabu).

 

 

 

 

فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ ﴿٣٢﴾

32. Kisha tukakupotoeni (kwa sababu) sisi (wenyewe) tulikuwa ni wenye kupotoka.

 

 

 

 

فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾

33. Basi hakika wao Siku hiyo, watashirikiana katika adhabu.  

 

 

 

 

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾

34. Hivyo ndivyo Tuwafanyavyo wahalifu.

 

 

 

 

 

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Wao walipokuwa wakiambiwa: Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah), wakitakabari.

 

 

 

 

 

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾

36. Na wanasema: Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?![3]

 

 

 

 

بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾

37. Bali (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa haki, na amewasadikisha Rusuli (waliotangulia).

 

 

 

 

إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ ﴿٣٨﴾

38. Hakika nyinyi (makafiri) bila shaka ni wenye kuionja adhabu iumizayo.

 

 

 

 

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na hamlipwi isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

 

إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾

40. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.

 

 

 

 

أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾

41. Hao watapata riziki maalumu.[4]

 

 

 

فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Matunda. Nao ni wenye kukirimiwa.

 

 

 

 

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٤٣﴾

43. Katika Jannaat za Neema.

 

 

 

 

عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٤﴾

44. Juu ya makochi ya enzi wakikabiliana.

 

 

 

 

يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿٤٥﴾

45. Wanazungushiwa gilasi za mvinyo kutoka chemchemu.

 

 

 

 

بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ ﴿٤٦﴾

46. Mweupe, wenye ladha kwa wanywaji.

 

 

 

 

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾

47. Hamna humo madhara yoyote, na wala wao kwayo hawataleweshwa.

 

 

 

 

وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ ﴿٤٨﴾

48. Na watakuwa nao wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, wenye macho mapana mazuri ya kuvutia. 

 

 

 

 

كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿٤٩﴾

49. (Wanyororo, watakasifu) kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhiwa.

 

 

 

 

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٥٠﴾

50. Basi watakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakiulizana.[5]

 

 

 

 

قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ ﴿٥١﴾

51. Aseme msemaji miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki mwandani.

 

 

 

 

 

يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ ﴿٥٢﴾

52. Aliyekuwa akiniambia: Je, hivi wewe ni miongoni mwa wanaosadiki?

 

 

 

 

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ ﴿٥٣﴾

53. Je tutakapokufa, tukawa udongo na mifupa, eti kweli sisi tutahukumiwa na kulipwa kikamilifu?

 

 

 

 

قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ﴿٥٤﴾

54. Atasema: Je, mngependa kuchungulia (nami motoni)?

 

 

 

 

فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٥٥﴾

55. Basi akapitisha macho, akamuona (rafiki yake) yuko katikati ya moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

قَالَ تَاللَّـهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ ﴿٥٦﴾

56. Akasema: Ta-Allaahi![6] Ulikaribia kuniangamiza!

 

 

 

وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٥٧﴾

57. Na lau kama si Neema ya Rabb wangu, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wahudhurishwao (motoni).

 

 

 

 

أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ ﴿٥٨﴾

58. Je, sisi hatutakufa tena?

 

 

 

 

إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٥٩﴾

59. Isipokuwa mauti yetu ya awali, nasi hatutaadhibiwa!  

 

 

 

 

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٠﴾

60. Hakika huku ndiko kufuzu kukubwa.

 

 

 

 

لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ ﴿٦١﴾

61. Kwa (ajili ya kupata) mfano wa haya basi watende wenye kutenda.

 

 

 

 

أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾

62. Je hiyo (Jannah) ni mapokezi bora, au mti wa zaqquwm (motoni)?[7]

 

 

 

 

إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾

63. Hakika Sisi Tumeufanya (zaqquwm) kuwa ni jaribio kwa madhalimu.

 

 

 

 

إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾

64. Hakika huo ni mti unaotoka katika kina cha moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾

65. Mashada ya matunda yake ni kana kwamba vichwa vya mashaytwaan.

 

 

 

 

فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾

66. Basi hakika wao, bila shaka watakula humo na watajaza matumbo yao kwayo.

 

 

 

 

ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٦٧﴾

67. Kisha hakika wao watapata mchanganyiko wa maji yachemkayo.

 

 

 

 

ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ ﴿٦٨﴾

68. Kisha marejeo yao bila shaka yatakuwa kuelekea kwenye moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ ﴿٦٩﴾

69. Hakika wao waliwakuta baba zao wamepotoka.

 

 

 

 

فَهُمْ عَلَىٰ آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ ﴿٧٠﴾

70. Na wao wakaharakiza kufuata athari zao. 

 

 

 

 

وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٧١﴾

71. Na kwa yakini walipotoka kabla yao watu wengi wa awali.

 

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ﴿٧٢﴾

72. Na kwa yakini Tuliwatumia waonyaji.

 

 

 

 

فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾

73. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya walioonywa?

 

 

 

 

إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾

74. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.[8]

 

 

 

 

وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ ﴿٧٥﴾

75. Na kwa yakini Nuwh alituita (Tumnusuru). Nasi kwa hakika Ni Waitikiaji bora kabisa.

 

 

 

 

وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾

76. Na Tukamuokoa pamoja na ahli zake kutokana na janga kubwa mno.

 

 

 

 

وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ ﴿٧٧﴾

77. Na Tukajaalia dhuria wake wao ndio wenye kubakia.[9]

 

 

 

 

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿٧٨﴾

78. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye. 

 

 

 

 

سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ ﴿٧٩﴾

79.  Salaamun! (Amani) iwe juu ya Nuwh ulimwenguni.

 

 

 

 

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٠﴾

80. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.[10]

 

 

 

 

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨١﴾

81. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.

 

 

 

 

ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٨٢﴾

82. Kisha Tukawagharikisha wengineo.

 

 

 

 

وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ ﴿٨٣﴾

83. Na hakika katika waliofuata njia yake (ya Tawhiyd) ni Ibraahiym.

 

 

 

 

إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٤﴾

84. Alipomjia Rabb wake kwa moyo uliosalimika.[11]

 

 

 

 

 

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ ﴿٨٥﴾

85. Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?

 

 

 

 

أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّـهِ تُرِيدُونَ ﴿٨٦﴾

86. Je, kwa uzushi tu, mnataka waabudiwa badala ya Allaah?

 

 

 

 

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾

87. Basi nini dhana yenu kuhusu Rabb wa walimwengu?

 

 

 

 

فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ ﴿٨٨﴾

88. Akatupa jicho juu mbinguni kutafakuri (udhuru wa kuwapa).

 

 

 

 

فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾

89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa.

 

 

 

 

فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾

90. Wakaachana naye wakimgeukilia mbali kwenda zao.

 

 

 

 

فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾

91. Akaenda kwa siri kwa waabudiwa wao, akasema: Mbona hamli? 

 

 

 

 

مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾

92. Mna nini! Mbona hamsemi?

 

 

 

 

فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ ﴿٩٣﴾

93. Akayakamia (masanamu) na kuyapiga kwa mkono wa kulia.

 

 

 

 

فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ﴿٩٤﴾

94.  Wakamjia mbio kwa vishindo.

 

 

 

 

قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ﴿٩٥﴾

95. Akasema: Je, mnaabudu vile mnavyovichonga?

 

 

 

 

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na hali Allaah Amekuumbeni pamoja na vile mnavyovifanya?

 

 

 

 

قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ ﴿٩٧﴾

97. Wakasema: Mjengeeni jengo, kisha mtupeni katika moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ ﴿٩٨﴾

98. Wakamkusudia njama, lakini Tukawafanya wao ndio wa chini kabisa. 

 

 

 

 

وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾

99. Akasema: Hakika mimi ni mwenye kwenda kwa Rabb wangu, Ataniongoza.

 

 

 

رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾

100. Rabb wangu!  Nitunukie miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

 

فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾

101. Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu.

 

 

 

 

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Alipofikia makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, akasema: Ee mwanangu! Hakika mimi naona njozi usingizini kwamba mimi nakuchinja, basi tazama, unaonaje? (Ismaa’iyl) akasema: Ee baba yangu kipenzi! Fanya yale unayoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri.

 

 

 

 

فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾

103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji.

 

 

 

 

وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾

104. Na tukamwita: Ee Ibraahiym.

 

 

 

 

قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾

105. Kwa yakini umesadikisha njozi. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾

106. Hakika hili bila shaka ni jaribio bayana.

 

 

 

 

وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾

107. Na Tukamtolea fidia kwa dhabihu adhimu.[12]

 

 

 

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.

 

 

 

سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾

109. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Ibraahiym.

 

 

 

كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾

110. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾

111. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.

 

 

 

 

وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٢﴾

112. Na Tukambashiria Is-haaq; Nabiy miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

 

وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰ إِسْحَاقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ مُبِينٌ ﴿١١٣﴾

113. Na Tukambarikia yeye na Is-haaq. Na katika vizazi vyao wawili kuna mhisani na aliyejidhulumu nafsi yake waziwazi.

 

 

 

وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١١٤﴾

114. Na kwa yakini Tuliwafanyia fadhila Muwsaa na Haaruwn.

 

 

 

 

وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿١١٥﴾

115. Na Tukawaokoa wote wawili na watu wao kutokana na janga kuu.[13]

 

 

 

وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٦﴾

116. Na Tukawanusuru, basi wakawa wao ndio wenye kushinda.

 

 

 

 

وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ ﴿١١٧﴾

117. Na Tukawapa Kitabu kinachojibainisha chenyewe waziwazi.

 

 

 

 

وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١١٨﴾

118. Na Tukawaongoza njia iliyonyooka.

 

 

 

 

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ ﴿١١٩﴾

119. Na Tukawaachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.

 

 

 

 

سَلَامٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٠﴾

120. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Muwsaa na Haaruwn.

 

 

 

 

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢١﴾

121. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٢﴾

122. Hakika wao wawili ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.

 

 

 

 

وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾

123. Na hakika Iliyaas[14] bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

 

 

إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Alipowaambia watu wake: Je, hamtokuwa na taqwa?

 

 

 

 

أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ ﴿١٢٥﴾

125. Mnamwomba ba’laa[15], na mnaacha Mbora wa wenye kuumba?  

 

 

 

 

 

اللَّـهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٢٦﴾

126. Allaah; Rabb wenu, na Rabb wa baba zenu wa awali.

 

 

 

 

فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Wakamkadhibisha. Basi wao bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).

 

 

 

إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٢٨﴾

128. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.

 

 

 

 

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٢٩﴾

129. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.

 

 

 

 

سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Ilyaasiyn.

 

 

 

 

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣١﴾

131. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾

132. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.

 

 

 

 

وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Na hakika Luutw bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

 

 

إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٣٤﴾

134. Tulipomuokoa pamoja na ahli zake wote.

 

 

 

 

إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Isipokuwa ajuza (bikizee) katika waliobakia nyuma.

 

 

 

 

ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٣٦﴾

136. Kisha Tukawadamirisha wengineo.

 

 

 

 

وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ ﴿١٣٧﴾

137. Nanyi bila shaka mnawapitia asubuhi.

 

 

 

 

وَبِاللَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na usiku. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

 

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾

139. Na hakika Yuwnus[16] bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

 

 

إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾

140. Alipokimbilia katika merikebu iliyosheheni.

 

 

 

 

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾

141. Akapiga kura ya vishale akawa miongoni mwa walioshindwa. 

 

 

 

 

فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾

142. Basi samaki mkubwa akammeza hali ya kuwa amefanya jambo la kulaumiwa.

 

 

 

فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Na lau kama hakuwa miongoni mwa wenye kumsabbih Allaah.

 

 

 

 

لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Angelibakia tumboni mwake mpaka Siku watakayofufuliwa.

 

 

 

 

فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾

145. Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (alipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa.

 

 

 

وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾

146. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mmung’unya.

 

 

 

وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾

147. Na Tukamtuma kwa (watu wake) laki moja au wanaozidi.

 

 

 

 

فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١٤٨﴾

148. Wakaamini, basi Tukawastarehesha kwa muda.  

 

 

 

 

فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ ﴿١٤٩﴾

149. Basi waulize (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, Rabb wako ndio ana mabanati, na wao ndio wana watoto wa kiume?[17]

 

 

 

أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Au, je Tumewaumba Malaika wanawake, nao wakawa ni wenye kushuhudia?

 

 

 

أَلَا إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ ﴿١٥١﴾

151. Tanabahi!  Hakika wao kwa uzushi wanasema:

 

 

 

وَلَدَ اللَّـهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٥٢﴾

152. Allaah Amezaa. Na hakika wao bila shaka ni waongo!

 

 

 

 

أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ ﴿١٥٣﴾

153. Je, Amekhitari mabanati kuliko wana wa kiume?

 

 

 

 

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Mna nini! Vipi mnahukumu?

 

 

 

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٥﴾

155. Je, hamkumbuki?

 

 

 

أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٥٦﴾

156. Je, mna hoja bayana (mnayodai)?

 

 

 

فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٥٧﴾

157. Basi leteni kitabu chenu mkiwa ni wakweli.

 

 

 

 

وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Na wakafanya baina Yake (Allaah) na baina ya majini unasaba. Na hali majini wamekwishajua kwamba kwa yakini wao, bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).[18]

 

 

 

سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Subhaana Allaah (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na yale wanayoyavumisha.

 

 

 

إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٠﴾

160. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.

 

 

 

 

فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ ﴿١٦١﴾

161. Basi hakika nyinyi na vile mnavyoabudu.

 

 

 

 

مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ ﴿١٦٢﴾

162. Hamuwezi kumpotosha yeyote.

 

 

 

 

إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ ﴿١٦٣﴾

163. Isipokuwa yule ambaye amehukumiwa kuingia na kuungua katika moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾

164. Na hakuna miongoni mwetu (Malaika) isipokuwa ana mahali maalumu.

 

 

 

وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾

165. Na hakika sisi bila shaka ni wenye kujipanga safu safu (kwa ibaada).

 

 

 

 

وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ ﴿١٦٦﴾

166. Na hakika sisi bila shaka ni wenye kumsabbih Allaah.

 

 

 

وَإِن كَانُوا لَيَقُولُونَ ﴿١٦٧﴾

167. Na hakika (washirikina) walikuwa wakisema:

 

 

 

 

لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦٨﴾

168. Lau tungelikuwa na ukumbusho kama walivyokuwa wa mwanzo.

 

 

 

 

لَكُنَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٩﴾

169. Bila shaka tungelikuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.

 

 

 

فَكَفَرُوا بِهِ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿١٧٠﴾

170. Lakini wakaikanusha (Qur-aan). Basi karibuni watakuja kujua.

 

 

 

 

وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧١﴾

171. Kwa yakini limekwishasabiki Neno Letu kwa Waja Wetu, Rusuli (waliotumwa).

 

 

 

 

إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنصُورُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Kwamba hakika wao bila shaka ndio wenye kunusuriwa.

 

 

 

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿١٧٣﴾

173. Na kwamba hakika Askari Wetu ndio watakaoshinda.

 

 

 

 

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٤﴾

174. Basi waachilie mbali mpaka muda.

 

 

 

وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٥﴾

175. Na watazame tu, nao karibuni watakuja ona.

 

 

 

أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٧٦﴾

176. Je, wanaharakiza Adhabu Yetu?

 

 

 

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٧﴾

177. Na itakapoteremka uwanjani mwao, basi ubaya ulioje wa asubuhi ya walioonywa!  

 

 

 

وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٨﴾

178. Na waachilie mbali mpaka muda.

 

 

وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٩﴾

179. Na tazama tu, nao karibuni watakuja ona.

 

 

 

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾

180. Utakasifu ni wa Rabb wako; Rabb wa Enzi Ya Nguvu Asiyeshindika kutokana na yale wanayoyavumisha.

 

 

 

وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾

181. Na Salaamun! (Amani) iwe juu ya Rusuli.

 

 

 

وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٢﴾

182. Na AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.

 

 

 

 

 

[1] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Mambo Matatu:

 

Rejea Suwrah hii Asw-Swaaffaat (37:10),  Al-An’aam (6:97), An-Nahl (16:16), Al-Mulk (67:5).

 

[2] Washirikina Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa:

 

Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.

 

[3] Makafiri Kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  Sifa Ovu:

 

Makafiri wa Kiquraysh hawakuacha kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  sifa ovu kama hizi, ilhali kabla ya kupewa Unabii walimwita kwa sifa njema kabisa ya Asw-Swiddiyq Al-Amiyn (mkweli mwaminifu).

 

Basi mara wamwite mshairi, mara majnuni, mara mchawi, mara kuhani,  mara mwongo na kadhalika. Rejea Swaad (38:4),  na zaidi rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi bayana na rejea mbalimbali za maudhui hii ya washirikina kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa kadhaa ovu na kuipachika Qur-aan pia sifa ovu. 

 

Na hii ilikuwa pia ni ada ya makafiri wa awali kuwapachika sifa ovu Rusuli wao. Rejea Adh-Dhaariyaat kwenye maelezo na rejea mbalimbali nyenginezo.

 

[4] Neema Za Watu Wa Jannah:

 

Aayah hii (41) hadi namba (49)  zinataja baadhi ya neema na raha za watu ndani ya Jannah. Rejea pia Faatwir (35:35) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.

 

[5] Shukurani Za Mtu Mwema Kutokumfuata Rafiki Mpotoshaji:

 

Kuanzia Aayah hii (50) hadi namba (57), zinaelezea kuhusu rafiki wawili; mwema na muovu mpotoshaji na shukurani za mwema alipoingia Jannah akamkuta rafiki mpotoshaji motoni.

 

Rejea Al-Furqaan (25:27-29) kwenye majuto ya mtu kufuata rafiki muovu.

 

[6]  (تَاللَّهِ)  Ta-Allaahi, (وَاللَّهِ) Wa-Allaahi,  (بِاللَّهِ)  Bi-Llaahi, Ni Kuapa Kwa Jina La Allaah.

 

Rejea An-Nahl (16:56) kwenye ufafanuzi.

 

[7] Mti Wa Zaqquwm:

 

Ni mti mchungu wa karaha kabisa motoni, na ni chakula cha wakaazi wa humo. Rejea Al-Israa (17:60), Ad-Dukhaan (44:43-46).

 

Rejea pia Faatwir (35:36) na An-Nabaa (78:21) kwenye fafanuzi, maelezo bayana na rejea mbalimbali za adhabu motoni.

 

[8] Waliokhitariwa Kwa Ikhlaasw Zao:

 

Aayah hii imekariri mara nne katika Suwrah hii baada ya kutajwa Rusuli kadhaa na watu wao. Tafsiyr yake ni:

 

Kwa vile walioonywa hawakuwa wote ni wapotofu, bali miongoni mwao wako walioamini na wakamtakasia Allaah Dini, basi hao Allaah Aliwaepusha na maangamizi ndipo Akasema:

إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾

“Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.”

 

Yaani: Ambao Allaah Aliwatakasa na Akawahusisha na Rehma Yake kutokana na wao kuwa na ikhlaasw Naye, na kwa sababu hiyo, mwisho wao umekuwa ni wenye kuhimidiwa. Kisha Akataja aina za adhabu za waliokadhibisha. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[9] Nuwh Na Kizazi Kilichobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Pili Kwa Wanaadam Baada Ya Aadam.

 

Baada ya Nuwh (عليه السّلام)  kupanda jahazi, akachukua kila kiumbe dume na jike kama Alivyoamrishwa na Allaah (سبحانه وتعالى), watu waliobakia wote pamoja na mwanawe waligharikishwa baharini, nao ni wale ambao walimkanusha Nuwh  (عليه السّلام) wakaendelea na ukafiri wao. 

 

Tafsiyr ya Aayah ni:

 

Na (Allaah) Akawazamisha makafiri wote, na Akawabakisha dhuria wake na kizazi chake kinachozaliana. Hivyo basi watu wote wametokana na dhuria wa Nuwh (عليه السّلام). Na Akamjaalia sifa njema hadi zama za wengine. Na hiyo ni kwa sababu yeye ni mwema katika kumwabudu Muumba, mkarimu kwa viumbe, na hii ni Desturi Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kwa wafanyao wema, kuwaenezea sifa nzuri kulingana na ihsaan zao. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Rejea Yuwnus (10:73), Huwd (11:40), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27).

 

Na pia rejea Suwrah Nuwh (71:1) kwenye maelezo kuwa Nuwh alikuwa ni Rasuli wa kwanza ardhini.

 

[10] Hakika Hivyo Ndivyo Tunavyowalipa Wafanyao Ihsaan:

 

Aayah hii imekariri mara nne baada ya kutajwa Rusuli kadhaa. Tafsiyr yake ni:

 

Hivi ndivyo Tunavyomlipa mja aliyefanya vyema katika kumtii Allaah. Tunamfanyia ukumbusho mzuri wa kutajwa na watu baada ya kufariki kwake kwa namna inayolingana na hadhi yake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[11] Moyo Uliosalimika:

 

Rejea Ash-Shu’araa (26:89) kwenye ufafanuzi wa moyo uliosalimika.

 

Kinyume cha moyo uliosalimika ni moyo ulio na maradhi. Rejea Muhammad (47:20) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:46) ambako kuna maelezo na ufafanuzi wa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾

Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.”

 

[12] Dhabihu Ndio Wanayochinja Waislamu Siku Ya ‘Iyd Al-Adhwhaa:

 

Rejea Alhidaaya.com > Fiqh-Ibaadah > Hajj > Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake.

 

[13] Janga Kuu Walilookolewa Nalo Nabiy Muwsaa Na Haaruwn (عليهما السّلام):

 

Na Tukawaokoa wao wawili na watu wao kutokana na gharika, utumwa na madhila waliokuwa nao (kutoka kwa Firawni). [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[14] Ilyaas:

 

Ni Rasuli Wa Kaumu Katika Bani Israaiyl.

 

[15] Ba’laa:

 

Jina la sanamu lao mahsusi lenye kumaanisha mola.

 

[16] Nabiy Yuwnus (عليه السّلام):

 

Yuwnus (عليه السّلام) ni miongoni mwa Manabii waliofadhilishwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((؟مَا يَنْبَغِى لِعَبْدٍ أَنْ يَقُولَ أَنَا خَيْرٌ مِنْ يُونُسَ بْنِ مَتَّى عَلَيْهِ السَّلاَمُ))

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Haipasi mja yeyote aseme kuwa mimi ni mbora kuliko Yuwnus ibn Mattaa (عليه السّلام).”   [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

[17] Washirikina Wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Malaika Ni Mabanaati Wake:

 

Aayah hii ya (149) hadi (159), zinahusiana na usingiziaji wa dhulma kubwa kuwa Allaah Ana wana wa kike, au Allaah Amezaa! Subhaanah wa Ta’aalaa (Ametakasika na Ametukuka kwa Uluwa) kutokana na wanayomsingizia!. Pia Rejea Al-Israa (17:40), Az-Zukhruf (43:15-19), An-Nahl (57-59).

 

Huu ni mgawanyo na kauli ya dhulma kubwa mno! Mgawanyo wa sehemu mbili: Upande mmoja wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana mwana wa kiume, na upande mwengine wamemsingizia kuwa Ana mabanaat (watoto wa kike) ambao wao wenyewe hawaridhii kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah An-Nahl (16:57):

 

وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾

“Na wanamfanyia Allaah kuwa ana mabinti! Utakasifu ni Wake! Na wao wawe na (wana wa kiume) wanaowatamani.”   [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Hawakuwa wakiwaridhia mabanaat kwa sababu ilikuwa wanapozaliwa wanawazika wazima wazima! Rejea An-Nahl (16:57-59), At-Takwiyr (81:8-9).

 

[18] Washirikina Na Makafiri Quraysh Wamemsingizia Allaah Kuwa Ana Mke Na Malaika Ni Mabinti Zake:

 

Allaah (عزّ وجلّ) Ametukuka kutokana na wanayomuelezea ya kumpachika mke na wana!  Na Allaah Awalaani na Awaadhibu kwa wanavyostahiki ya kumzulia Kwake hivyo, Awaangamizilie mbali! Tunakiri kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Hana mke wala hana mwana, bali Yeye ni Al-Waahid (Pekee) Asiyezaa wala Asiyezaliwa, Yeye ni Al-Ghaniyyu (Mkwasi Hahitaji lolote). Subhaana Allaah wa Ta’aala Ametukuka kwa ‘Uluwa Adhimu kabisa kutokana na kila wanalomzulia.

 

Washirikina (makafiri wa Kiquraysh wa Makkah) walimpachika Allaah (عزّ وجلّ) unasaba baina Yake na majini kutokana na madai yao kuwa Malaika ni mabinti wa Allaah. Walipoulizwa nani mama yao hao Malaika ambao wanamsingizia kuwa ni mabinti Wake (kwani hakuna budi kuweko mama aliowazaa)? Wakajibu kuwa mama yao hao Malaika ni mabinti wa wakuu wa majini, yaani watukufu wao na mabwana zao. [Tafsiyr As-Sa’diy, Ibn Kathiyr]

 

Baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan wameona kwamba ingawa neno lililotumika katika Aayah ni al-jinnah (majini), lakini hapo waliokusudiwa ni Malaika. Wakatoa maoni kwamba hapa neno al-jinnah (majini) limekusudiwa kwa maana yake halisi (ya uumbaji uliofichika), na kwamba Malaika pia ni viumbe vilivyofichika. Lakini hiyo si kauli sahihi bali ilokusudiwa hapo ni majini wenyewe. [Tafsiyr Suwrah Asw-Swaaffaat – Imaam Muhammad Bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn]

 

 

 

Share