076 - Al-Insaan

 

  الإِنْسَان

 

076-Al-Insaan

 

076-Al-Insaan: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا﴿١﴾

1. Kwa hakika kilimpitia binaadam kipindi fulani katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa.

 

 

 

إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا﴿٢﴾

2. Hakika Sisi Tumemuumba binaadam kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu, Tukamfanya mwenye kusikia na mwenye kuona.

 

 

 

إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾

3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwingi wa kukufuru.[1]

 

 

 

إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا﴿٤﴾

4. Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na moto uliowashwa vikali mno.

 

 

 

إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا﴿٥﴾

5. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi watakunywa katika vikombe vya mvinyo, mchanganyiko wake ni kaafuwr.[2]

 

 

 

 

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا﴿٦﴾

6. Nayo ni chemchemu watakayokunywa toka humo Waja wa Allaah, wataibubujua kwa wingi.

 

 

 

 

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾

7. Wanatimiza nadhiri[3] na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana.

 

 

 

 

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾

8. Na wanalisha chakula, juu ya kuwa wao wanakipenda, masikini na mayatima na mateka.[4]

 

 

 

 

إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾

9. Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kutoka kwenu jazaa wala shukurani.

 

 

 

 

إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا﴿١٠﴾

10. Hakika sisi tunaikhofu kutoka kwa Rabb wetu siku ya masononeko, ngumu na ndefu mno.

 

 

 

 

فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا﴿١١﴾

11.  Basi Allaah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawapa nuru ya ujamali na furaha.

 

 

 

 

وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا﴿١٢﴾

12. Na Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Jannah na nguo za hariri.

 

 

 

 

مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا﴿١٣﴾

13. Wataegemea humo juu ya makochi ya fakhari, hawatoona humo joto la jua wala baridi kali.

 

 

 

 

وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا﴿١٤﴾

14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao na yatainamishwa matunda yake ya kuchumwa, yawakurubie.

 

 

 

 

وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا﴿١٥﴾

15. Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri za vigae.

 

 

 

 

قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا﴿١٦﴾

16. Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo.

 

 

 

 

وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا﴿١٧﴾

17. Na watanyweshwa humo kikombe cha mvinyo ambao mchanganyiko wake ni tangawizi.

 

 

 

 

عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا﴿١٨﴾

18. (Mvinyo utokao) chemchemu iliyomo humo inayoitwa Salsabiyl.

 

 

 

 

وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا﴿١٩﴾

19. Na watawazungukia wavulana wa kudumishwa, utakapowaona, utawadhania ni lulu zilizotawanywa.

 

 

 

 

 

وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا﴿٢٠﴾

20. Na utakapoona huko, utaona neema na ufalme adhimu.

 

 

 

 

عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا﴿٢١﴾

21. Juu yao watavaa nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel, na watapambwa vikuku vya fedha,[5] na Rabb wao Atawanywesha kinywaji kitwaharifu.

 

 

 

إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا﴿٢٢﴾

22. (Wataambiwa): Hakika haya ni jazaa yenu, kwani juhudi zenu zimethaminiwa.

 

 

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا﴿٢٣﴾

23. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Qur-aan uteremsho wa hatua kwa hatua.

 

 

 

 

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا﴿٢٤﴾

24. Basi fanya subira kwa Hukumu ya Rabb wako, na wala usimtii miongoni mwao atendaye dhambi au mwingi wa kukufuru.

 

 

 

 

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾

25. Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni.[6]

 

 

 

 

وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾

26. Na katika sehemu ya usiku msujudie, na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu.[7]

 

 

 

إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا﴿٢٧﴾

27. Hakika hawa wanapenda uhai wa dunia na wanaacha nyuma yao siku nzito (ya Qiyamaah).

 

 

 

نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا﴿٢٨﴾

28. Sisi Tumewaumba, na Tumetia nguvu viungo vyao. Na kama Tukitaka, Tutawabadilisha mfano wao badala yao.

 

 

 

إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿٢٩﴾

29. Hakika haya ni mawaidha. Basi anayetaka achukue njia ya kuelekea kwa Rabb wake.

 

 

 

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾

30. Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٣١﴾

31. Anamuingiza Amtakaye katika Rehma Yake, na madhalimu Amewaandalia adhabu iumizayo.

 

 

 

 

[1] Njia Mbili: Ya Hidaaya Na Ya Upotofu:

 

Kila kizazi kimeumbwa katika Fitwrah (maumbile ya asili) ya kumwabudu na kumtii Muumba wake kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا يُولَدُ عَلَى الْفِطْرَةِ  فَأَبَوَاهُ يُهَوِّدَانِهِ ، وَيُنَصِّرَانِهِ  وَيُمَجِّسَانِهِ  كَمَا تُنْتَجُ  الْبَهِيمَةُ بَهِيمَةً جَمْعَاءَ ، هَلْ تُحِسُّونَ فِيهَا مِنْ جَدْعَاءَ؟)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ:  وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ))  

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema; “Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika fitwrah (umbile la asili la utiifu) kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswaara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe? Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (kauli ya Allaah):

 

  فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ

 “(Shikamana na) umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu. Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah.” [Ar-Ruwm (30:30) Hadiyth katika Al-Bukhaariy na Muslim]     

 

Rejea katika tanbihi ya Aayah hiyo kwenye faida nyenginezo

 

Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawabainishia wanaadam njia mbili; njia ya hidaaya na njia ya upotofu kwa kuwatuma Rusuli Wake na Risala Yake kuwabalighishia watu. Basi hii ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾

“Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)?” [Al-Balad (90:10)]

 

Basi ni juu ya mwanaadam kuchagua njia anayotaka. Akiwa ni mtu mwenye kumkhofu Allaah Akafuata Amri zake, basi huyo amejichagulia njia ya hidaaya. Na akiwa ni mtu anayefuata matamanio yake akakufuru au kumuasi Allaah, basi huyu amejichagulia mwenyewe upotofu. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ametoa mfano wa waliostahabu upotofu badala ya hidaaya kama kina Thamuwd watu wa Nabiy Swaalih (عليه السّلام):

وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾

“Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya. Basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa sababu ya waliyokuwa wakiyachuma.” [Fusw-Swilat (41:17)]

 

[2] Sifa Za Al-Abraar (Watendao Wema Kwa Wingi) Na Jazaa Zao:

 

Kuanzia Aayah hii namba (5) hadi namba (22) zimetajwa sifa za Al-Abraar (Waja wema wenye kutenda wema wa kila aina kwa wingi) pamoja na jazaa zao walizoandaliwa na Allaah (سبحانه وتعالى) katika Jannah.

 

Rejea pia Faatwir (35:33) kwenye neema nyenginezo za watu watu wa Jannah, pamoja na rejea nyenginezo mbalimbali za neema za watu wa Jannah.  

 

[3] Kutimiza Nadhiri:

 

Muumini anapoweka nadhiri ya kufanya jambo la utiifu na la kheri, anapaswa kuitimiza. Lakini anapoweka nadhiri ya jambo la uasi, anapaswa kutokutimiza kama alivyotuamrisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيعَ اللَّهَ فَلْيُطِعْهُ وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اللَّهَ فَلاَ يَعْصِهِ ‏"‏ ‏.‏

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii, na mwenye kuweka nadhiri kwamba atamuasi Allaah, basi asimuasi.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6696), Abu Daawuwd (3289), At-Tirmidhiy (1526), An-Nasaaiy (7/17) na Ibn Maajah (2126)]

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida kuhusu somo la nadhiri na viapo:

 

13-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Yamini (Viapo) Na Nadhiri - كِتَابُ اَلْأَيْمَانُ وَالنُّذُورُ

 

07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ الأيمان وَالنُّذور - Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

[4] Kulisha Chakula Ni Miongoni Mwa Sababu Mojawapo Ya Kuingizwa Jannah:

 

Mojawapo ya mafundisho ya mwanzo kabisa ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Madiynah, yalikuwa ni kuhimiza kulisha watu chakula, ikaahidiwa mwenye kufanya hivyo kuwa ataingizwa Jannah. Hadiyth ifuatayo imethibitisha:

 

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ سَلَّامٍ ‏- رضى الله عنه ‏- قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏- صلى الله عليه وسلم ‏-  يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ! أَفْشُوا اَلسَّلَام، وَصِلُوا اَلْأَرْحَامَ، وَأَطْعِمُوا اَلطَّعَامَ، وَصَلُّوا بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا اَلْجَنَّةَ بِسَلَامٍ   أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِي

  

Amesimulia ‘Abdullaah bin Sallaam (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, enezeni (amkianeni) salaam, na ungeni undugu wa damu, na lisheni chakula, na Swalini watu wakiwa wamelala, mtaingia Jannah kwa amani.” [At-Tirmidhiy]

 

Rejea pia Al-Qalam (68:17) kwenye kisa cha watu wa shamba waliozuia mafuqara na masikini wasipate swadaqa ya mazao ya shamba la baba yao baada ya kufariki kwake. Na pia kisa katika Hadiyth, cha mtu aliyekuwa akitoa swadaqa mazao yake, na faida nyenginezo.

 

[5]  Mavazi Ya Watu Wa Jannah Na Mavazi Yaliyoharamishwa Duniani:

 

Mavazi ya watu wa Jannah yatakuwa ni nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel, na watapambwa vikuku vya fedha.

 

Rejea pia Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى): Al-Hajj (22:23), Al-Kahf (18:30-31).

 

Lakini nguo za hariri zimeharamishwa kwa wanaume kuzivaa duniani. Hali kadhaalika imeharamishwa kutumia vyombo vya dhahabu duniani kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سَيْفُ بْنُ أَبِي سُلَيْمَانَ، قَالَ سَمِعْتُ مُجَاهِدًا، يَقُولُ حَدَّثَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي لَيْلَى، أَنَّهُمْ كَانُوا عِنْدَ حُذَيْفَةَ فَاسْتَسْقَى فَسَقَاهُ مَجُوسِيٌّ‏.‏ فَلَمَّا وَضَعَ الْقَدَحَ فِي يَدِهِ رَمَاهُ بِهِ وَقَالَ لَوْلاَ أَنِّي نَهَيْتُهُ غَيْرَ مَرَّةٍ وَلاَ مَرَّتَيْنِ‏.‏ كَأَنَّهُ يَقُولُ لَمْ أَفْعَلْ هَذَا، وَلَكِنِّي سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ لاَ تَلْبَسُوا الْحَرِيرَ وَلاَ الدِّيبَاجَ وَلاَ تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَلاَ تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَنَا فِي الآخِرَةِ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Mujaahid (رضي الله عنه): ‘Abdur-Rahman bin Abi Laylaa (رضي الله عنه) amemuhadithia: Tulikuwa kwa Hudhayfah (رضي الله عنه) naye akaomba maji ya kunywa, na Mmajusi (muabudu moto) akamletea. Alipoliweka gudulia la maji mkononi mwake alimrushia nalo, na akasema: Kama nisingalimkataza kufanya hivi zaidi ya mara moja au mara mbili (nisingelimrushia nalo). Kama vile anasema nisingalifanya hivi. Lakini nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Msivae hariri wala dibaji na msinywe katika chombo cha dhahabu na fedha, na msile katika sahani zake, kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyetu Aakhirah” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Vyakula (70)]

 

Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:

 

08F-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: الآنِيَةُ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهَا - Vyombo Na Yanayohusiana

 

 

09A-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume

 

 

09B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: لِبَاسُ المَرْأَةِ Kivazi Cha Mwanamke

 

007-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Kuvaa Hariri Safi Isiyochanganywa

 

010-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Ya Rangi Ya Zafarani

 

07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Mwanamke Anaruhusiwa Kuvaa Hariri

 

133-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Makatazo Ya Kuvaa Hariri, Diybaaj (Hariri Iliyotariziwa) Na Kunywa Katika Vyombo Vya Dhahabu Na Fedha

 

111-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kutumia Vyombo vya Dhahabu, Fedha katika Kula, Kunywa, Tohara na Njia Zote za Matumizi yake

 

[6] Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) Mchana Na Usiku:

 

Tafsiyr:

 

Yaani: Mwanzo wa siku na mwisho wa siku, kwa hiyo inajumuisha Swalaah za faradhi na Swalaah za nawaafil (khiari) zinazofuatia, na Dhikr (kumdhukuru Allaah kwa kila aina ya dhikr kama Qur-aan), Tasbiyh, Tahliyl, Takbiyr katika nyakati hizi. [Tafsiyr As-Sa;diy]

 

Hivyo ni sawa na kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) nyakati zote. Rejea Al-Ahzaab (33:41) kwenye fadhila za kumdhukuru Allaah. Na Rejea Twaahaa (20:124) kwenye maonyo ya kughafilika na kumdhukuru Allaah. 

 

Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye adhkaar za asubuhi na jioni:

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

130-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl Na Takbiyr

 

131-Hiswnul-Muslim: Vipi Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akimsabihi Allaah

 

[7]  Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku) Kwa Ajili Ya Ibaada:

 

Rejea Al-Muzzammil (73:2) kwenye faida za somo hili.

 

 

 

 

Share