096 - Al-'Alaq

  الْعَلَق

 

096-Al-‘Alaq

 

096-Al-‘Alaq: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.[1]

 

 

 

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

2. Amemuumba binaadam kutokana na pande la damu linaloning’inia.

 

 

 

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

3. Soma. Kwani Rabb wako Ni Mkarimu kushinda wote.

 

 

 

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾

 

4. Ambaye Amefunza kwa kalamu.

 

 

عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

5. Amemfunza binaadamu asiyoyajua.

 

 

 

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾

6. Laa hasha! Hakika binaadamu bila shaka hupindukia mipaka kuasi.[2]

 

 

 

أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

7. Anapojiona kuwa amejitosheleza. 

 

 

 

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Hakika kwa Rabb wako ndio marejeo.

 

 

 

 

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾

9. Je, umemuona yule anayemkataza?

 

 

 

 

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Mja pale anaposwali?

 

 

 

 

أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾

11. Je umeona, ikiwa (huyu mwovu) atafuata uongofu.

 

 

 

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾

12. Au akalingania taqwa (si ingelikuwa bora zaidi kwake?)

 

 

 

 

أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾

13. Je umeona, kama ataendelea kukadhibisha na kukengeuka (si ataishilia pabaya?

 

 

 

 

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾

14. Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?

 

 

 

 

كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾

15. Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa shungi la nywele.

 

 

 

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾

16. Shungi la uwongo, lenye hatia.

 

 

 

فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾

17. Basi na aite timu yake.

 

 

 

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾

18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah (Malaika wa adhabu).[3]

 

 

 

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾

19. Laa hasha! Usimtii. Na sujudu na kurubia (kwa Allaah). 

 

 

 

[1] Mwanzo Kabisa Wa Wahy Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Aayah namba (1) hadi namba (5) ni za mwanzo kabisa kuteremshiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Wahy. Hadiyth ifuatayo inaelezea tukio hilo alipokuwa katika pango la Hiraa akitafakari Uumbaji wa Allaah:

 

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ ـ وَهُوَ التَّعَبُّدُ اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ الْعَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ، فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الْحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ الْمَلَكُ فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قَالَ ‏"‏ مَا أَنَا بِقَارِئٍ ‏"‏‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ فَقُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ ‏{‏اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ‏}‏ ‏"‏‏.‏ فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رضى الله عنها فَقَالَ ‏"‏ زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي ‏"‏‏.‏ فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الْخَبَرَ ‏"‏ لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي ‏"‏‏.‏ فَقَالَتْ خَدِيجَةُ كَلاَّ وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الْكَلَّ، وَتَكْسِبُ الْمَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الْحَقِّ‏.‏ فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ ـ وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الْكِتَابَ الْعِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالْعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ يَا ابْنَ عَمِّ اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ يَا ابْنَ أَخِي مَاذَا تَرَى فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَبَرَ مَا رَأَى‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى صلى الله عليه وسلم يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَوَمُخْرِجِيَّ هُمْ ‏"‏‏.‏ قَالَ نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلاَّ عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا‏.‏ ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ وَفَتَرَ الْوَحْىُ‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah Mama wa Waumini: Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa njozi njema usingizini, na alikuwa haoni njozi isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana. Kisha alipendezeshwa kujitenga, na alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akimwabudu (Allaah Pekee) mfululizo kwa siku nyingi kabla ya kwenda kwa familia yake kuchukua mahitajio ya kuweza kurudi tena huko na kisha alirejea kwa (mkewe) Khadiyjah (رضي الله عنها)  kuchukua chakula tena mpaka ukweli ulipomjia akiwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika alimjia na alimtaka asome. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Akajibu: “Mimi sio msomaji.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kusema: “Malaika akanishika kwa nguvu na akaniminya kwa nguvu mpaka nikapata tabu. Kisha aliniachia, na tena akanitaka nisome na nikamjibu: Mimi si msomaji. Akaniminya vile vile. Baada ya hapo akanishika tena akaniminya kwa mara ya tatu mpaka nikapata taabu. Kisha akaniachia akasema:

 

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba. Amemuumba binaadam kutokana na pande la damu linaloning’inia. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote. [Al-‘Alaq (96:1-3)]

 

Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alirejea na Wahy, na huku moyo ukidunda kwa nguvu. Kisha alikwenda kwa Khadiyjah bint Khuwaylid (رضي الله عنها) akasema, “Nifunikeni! Nifunikeni” Wakamfunika mpaka hofu ikatoweka, kisha akamueleza kila kitu kilichojiri akasema, “Naogopa nafsi yangu, kuna kitu (kibaya) kinaweza kunitokea.” “Khadiyjah (رضي الله عنها) akajibu, “Hapana kamwe! Wa-Allaahi, Allaah Hatokudhalilisha. Wewe una mahusiano mazuri na ndugu na marafiki, na unawasaidia masikini na mafukara, unawakirimu wageni wako na unawasaidia waliofikwa na majanga.” Kisha Khadiyjah (رضي الله عنها) alifuatana naye kwa binami yake, Waraqah bin Nawfal bin Asad bin Abdil-‘Uzzah, ambaye wakati wa Jahiliyya (kabla ya Uislam) alikuwa Mkristo na alikuwa akiandika kwa hati za Hebrew. Aliandika kutoka Injiyl kwa Hebrew kiasi alichowezeshwa na Allaah. Alikuwa mzee na alipoteza uoni (kipofu). Khadiyjah (رضي الله عنها) alimwambia Waraqah: “Sikiliza Hadithi (kisa) ya mpwa wako. Ee binami yangu!” “Waraqah akauliza, “Ee mpwa wangu! Umeona nini?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alielezea yote aliyoyaona. Waraqah akasema, “Huyu ni yule yule anayehifadhi siri (Malaika Jibriyl) ambaye Allaah alimpeleka kwa Muwsaa. Natamani ningekuwa kijana, na niishi mpaka pale watu wako watakapokufukuza.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza, “Je, Watanifukuza?” Waraqah akasema, “Mtu yeyote aliyeleta kitu kama ulicholeta alikabiliwa na misukosuko; na kama nitaikuta siku utakayofanyiwa uadui nitakuhami kwa nguvu zote.” Lakini baada ya siku chache Waraqah alifariki dunia na Wahyi ulisita kwa muda. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Wahy (1)]

 

[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

096-Asbaabun-Nuzuwl: Al-'Alaq Aayah 06-19: كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ

 

[3] Malaika Wa Adhabu Wangemkamata Abu Jahl Kama Angelimzuia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuswali Kwenye Ka’bah:

 

  عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ قَالَ أَبُو جَهْلٍ لَئِنْ رَأَيْتُ مُحَمَّدًا يُصَلِّي عِنْدَ الْكَعْبَةِ لأَطَأَنَّ عَلَى عُنُقِهِ‏.‏ فَبَلَغَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏ "‏ لَوْ فَعَلَهُ لأَخَذَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ  

Amesimulia ‘Ikrimah (رضي الله عنه): Abu Jahl alisema: Naapa, lau nitamuona Muhammad akiswali kwenye Al-Ka‘bah, nitamkanyanga shingo yake. Pindi khabari hiyo ilipomfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Lau atafanya hivyo, Malaika watamkamata.” [Al-Bukhaariy Kitabu cha Tafsiyr (65)]

 

 

 

 

Share