Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukmu Ya Kutupa Jalalani Chakula Kilichobakia

 

 

Hukmu Ya Kutupa Jalalani Chakula Kilichobakia

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya wanafuzi kutupa jalalani chakula au kinywaji kilichobakia?

 

 

JIBU:

 

Chakula ambacho hakiwezi kuliwa, kama maganda ya machungwa, ya tufaha na mabaki yake, au ndizi na mengineyo kama hayo, hakuna ubaya (kuyatupa) kwa sababu hayo hayana uharamu kwa vile yalivyo.

 

Ama chakula ambacho cha kuliwa kama mkate, mchuzi, na kama hivi basi havifai kutupwa katika pipa la taka, na ikibidi (kutupwa) basi vitiwe katika mfuko ili mchukuaji taka ajue kuwa hicho ni kitu chenye kuheshimiwa.

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn

[Fataawaa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (6/205)]

 

 

 

Share