005-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AR-RAHIYM

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

الرَّحِيم

 

005 - AR-RAHIYM

 

 

 

AR-RAHIYM: Mwenye kurehemu:

 

Sifa mbili za Rahmaan na Rahiym zinatokana na herufi tatu za asili na hivyo maana zake ni moja, isipokuwa tu kama ilivyobainishwa katika Sifa ya Rahmaan kwamba maana yake ni pana na inaenea zaidi kwa viumbe wote; Waumini kwa makafiri, watu wema kwa watu waovu. Ama Rahiym ni Sifa khaswa kwa ajili ya Waumini pekee kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

Naye kwa Waumini daima ni Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 43]

 

Na Anasema kuhusu waja Wake:

نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٤٩﴾

(Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Wajulishe waja Wangu, kwamba: Hakika Mimi ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Hijr: 49]

 

 Na pia kuhusu Maswahaba waliorudi kutubia:

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (vita vya Tabuwk) baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [At-Tawabah: 117]

 

Na Waumini watakapoingia Jannah:

إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.

 

هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾

Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.

 

لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾

Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.

 

سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

“Salaamun”; kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58]

 

Na pia katika hali nyingine ya Waumini wanapofishwa na kubashiriwa Jannah:

 

 إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٣٠﴾

30. Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (wanapofishwa kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”

 

نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ﴿٣١﴾

31. “Sisi ni marafiki walinzi wenu katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.

 

نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ ﴿٣٢﴾

32. “Ni takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Fusw-Swilat: 30-32]

 

Na katika du’aa, Anas bin Maalik amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Mu’aadh bin Jabal:

 

 "أَلا أُعَلِّمُكَ دُعَاءً تَدْعُو بِهِ لَوْ كَانَ عَلَيْكَ مِثْلُ جَبَلٍ دَيْنًا لأَدَّى اللهُ عَنْكَ؟ قُلْ يَا مُعَاذُ: اللَّهُمَّ مَالِكُ الْمُلْكِ، تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ، وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ، وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ، وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ، بِيَدِكَ الْخَيْرِ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، رَحْمَانُ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، تُعْطِيهُمَا مَنْ تَشَاءُ، وَتَمْنَعُ مِنْهُمَا مَنْ تَشَاءُ، ارْحَمْنِي رَحْمَةً تُغْنِينِي بِهَا عَنْ رَحْمَةِ مَنْ سِوَاكَ"

((Je, nikufundishe duaa ambayo ukiiomba basi ikiwa una deni mfano wa mlima wa Uhud, Allaah Atakukidhia.  Sema ya Mu’aadh: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. Mwingi wa rahmah duniani na Aakhirah Mwenye kurehemu, Unampa rahmah mbili hizo Umtakaye na Unamnyima Umtakaye. Nirehemu rahmah itakayonitosheleza kwayo rahmah isiyotoka kwa mwengine isipokuwa Wewe.)) [Hadiyth Hasan - Swahiyh At-Targhiyb (1821)]

 

Na pia Akaihusisha sifa hiyo kwa mja Wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, ni yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini (muongoke) mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]

 

Hivyo Waumini ni wenye neema na jina hili la Ar-Rahiym na lile la Ar-Rahman kama ilivyo katika Hadiyth: ((…Atakamilisha rahmah mia moja kwa mawalii Wake siku ya Qiyaamah)) [Hadiyth Swahiyh kwa sharti la Shaykhaan; Al-Bukhaariy na Muslim - angalia ‘Zawaaid Al-Muwatwaa na Al-Musnad 1/53].

 

Na Sifa au Majina haya mawili yametajwa katika Qur-aan kwa pamoja katika Aayah kadhaa mfano:

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163. “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” [Al-Baqarah: 163]

 

حم ﴿١﴾

Haa Miym.

 

 

تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٢﴾

Ni uteremsho kutoka kwa Mwingi wa Rahmah, Mwenye kurehemu. [Fusw-Swilat: 1-2]

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu. [Al-Hashr: 22]

 

Ama Sifa ya Rahiym imetajwa pamoja na Sifa au Majina Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mbali mbali khaswa pamoja na Al-Ghafuwr (Mwingi wa kufughuria) na Al-‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika). Mifano michache:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  [Aal-‘Imraan: 31]

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake, na kwamba Allaah ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [An-Nuwr: 20]

 

وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ ﴿٩٠﴾

“Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo khalisi.”  [Huwd: 20]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

Enyi mlioamini! Jieupusheni sana na dhana kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msifanyiane ujasusi, na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [Al-Hujuraat: 12]

 

بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾

Kwa nusura ya Allaah. Anamnusuru Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu. [Ar-Ruwm: 5]

 

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi wa huruma na fadhila, Mwenye kurehemu.” [Atw-Twuwr: 28]

 

 

 

 

 

Share