Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad: Maulidi: Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah
Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah Kama Ya Mawlid
Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, inafaa kula chakula cha watu wa bid’ah kwa kujua kwamba wanaandaa chakula hicho kwa ajili ya bid’ah hiyo, kama kuandaa chakula cha mawlid ya Nabiy?
JIBU:
Ni waajib kuwatanabahisha kwamba wanavuka mipaka katika bid’ah, na kwamba wasifanye yaliyoharamishwa.
Na mtu hatakiwi kula chakula kinachoandaliwa kwa ajili ya mambo ya bid’ah na mambo yaliyoharamishwa.
Kwa hiyo hapasi mtu kutumia chakula hicho bali inampasa atanabahi na atahadhari kuingia katika mambo hayo yaliyoharamishwa.
[Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad