195-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 195: وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 195: Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi...
وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾
195.
Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzia) mikono yenu isitoe. Na fanyeni ihsaan Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kuwazungumzia baadhi ya Swahaba ambao walikusudia kurudi ili kutengeneza mashamba yao na mali zao na waache Jihaad. [At-Tirmidhiy kutoka kwa Abuu Ayyuwb (رضي الله عنه)]
Pia, imeteremka kwa wale ambao walikuwa wakijitolea swadaqah (ambapo walikuwa) wanatoa vile ambavyo Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaka. Lakini pindi walipopatwa na ukame, walijizuia kutoa. [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Abuu Jubayrah (رضي الله عنه)]
Vile vile, mtu kati yao alipokuwa akifanya madhambi husema: “Allaah Hatonisamehe mimi.” [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Nu’maan (رضي الله عنه)]
Hadiyth yake ni kama ifuatavyo:
عَنْ أَسْلَمَ أَبِي عِمْرَانَ التُّجِيبِيِّ، قَالَ كُنَّا بِمَدِينَةِ الرُّومِ فَأَخْرَجُوا إِلَيْنَا صَفًّا عَظِيمًا مِنَ الرُّومِ، فَخَرَجَ إِلَيْهِمْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ مِثْلُهُمْ أَوْ أَكْثَرُ، وَعَلَى أَهْلِ مِصْرَ عُقْبَةُ بْنُ عَامِرٍ وَعَلَى الْجَمَاعَةِ فَضَالَةُ بْنُ عُبَيْدٍ، فَحَمَلَ رَجُلٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ عَلَى صَفِّ الرُّومِ حَتَّى دَخَلَ فِيهِمْ، فَصَاحَ النَّاسُ وَقَالُوا: سُبْحَانَ اللَّهِ يُلْقِي بِيَدَيْهِ إِلَى التَّهْلُكَةِ، فَقَامَ أَبُو أَيُّوبَ الأَنْصَارِيُّ فَقَالَ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ تَتَأَوَّلُونَ هَذِهِ الآيَةَ هَذَا التَّأْوِيلَ وَإِنَّمَا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِينَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ، لَمَّا أَعَزَّ اللَّهُ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَقَالَ بَعْضُنَا لِبَعْضٍ سِرًّا دُونَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: إِنَّ أَمْوَالَنَا قَدْ ضَاعَتْ وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ أَعَزَّ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَلَوْ أَقَمْنَا فِي أَمْوَالِنَا فَأَصْلَحْنَا مَا ضَاعَ مِنْهَا. فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم يَرُدُّ عَلَيْنَا مَا قُلْنَا: ((وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلاَ تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ)) فَكَانَتِ التَّهْلُكَةُ الإِقَامَةَ عَلَى الأَمْوَالِ وَإِصْلاَحَهَا، وَتَرَكْنَا الْغَزْوَ فَمَا زَالَ أَبُو أَيُّوبَ شَاخِصًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ حَتَّى دُفِنَ بِأَرْضِ الرُّومِ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ .
Imepokelewa kutoka kwa Aslam bin ‘Imraan At-Tujiybiyy (رضي الله عنه) kwamba: Tulikuwa mji wa Rumi, wakatujia safu kubwa ya Warumi. Basi Waislamu waliokaribia idadi yao au zaidi yake waliwaendea. ‘Uqbah bin ‘Aamir alikuwa ni Amiri wa Miswr, na Amiri wetu alikuwa ni Fadhwaalah bin ‘Ubayd. Mmoja miongoni mwa Waislamu alifikia safu ya Warumi mpaka akaingia kwao, watu wakapiga kelele: “Subhaana-Allaah! Amejitupa katika maangamizi! Abuu Ayyuwb Al-Answaariy akasema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnafasiri Aayah hii na hali Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi hadhara ya Answaariy pale Allaah Alipoupa nguvu Uislamu wakazidi wasaidizi wake. Baadhi yetu wakaambizana siri bila ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba: Mali zenu zimepotea na kwamba Allaah Ameutia nguvu Uislamu na wamezidi wasaidizi wetu. Hivyo tungelitunza mali zetu, ingelikuwa ni mbadala wa mali tuliyopoteza. Hapo Allaah Akamteremshia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kutukanya yale tuliyoyasema: “
Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzia) mikono yenu isitoe…” Basi maangamizi yakawa ni vile kutunza mali na kuzihifadhi. Tukaondoka vitani basi Abuu Ayyuwb hakuacha lengo la kupigana kwa ajili ya Allaah mpaka akazikwa katika ardhi ya Warumi. [Abuu 'Iysaa At-Tirmidhiy, amesema hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh Ghariyb, Taz. Swahiyh At-Targhiyb (1388)]