Imaam Ibn Baaz: Lipi Lilokuwa Bora Baina Kuisoma Qur-aan Na Kuisikiliza

Lipi Lilokuwa Bora Baina Kuisoma Qur-aan Na Kuisikiliza

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Lipi lilo bora kati ya mawili; Kuisoma Qur-aan au kuisikiliza kutoka kwa mmoja wa wasomaji wanaosoma kupitia kanda za sauti?

 

 

JIBU:

 

Bora zaidi afanye lile ambalo linalotengeneza moyo wake na ambalo lina taathira zaidi kati ya kuisoma au kuisikilza, kwa sababu linalokusudiwa ni kutadaburi (kuzingatia) na kuifahamu maana na kufanyia kazi yale ambayo Kitabu cha Allaah (‘Azza wa Jalla) kinamwongoza mtu afanye kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu):

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili. [Swaad 38: 29]

 

Na Anasema (‘Azza wa Jalla):

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ  

Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa… [Al-Israa 17: 9]

 

Na Anasema (Subhaanahu):

قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ  

Sema: “Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa… [Fusw-Swilat 41: 44]

 

 

[Fataawa Imaam Ibn Baazhttps://www.binbaz.org.sa/fatawa/1053]

 

 

Share