Du'aa Mbalimbali Anazozihitaji Muislamu Kuzifahamu (Pamoja Na Matamshi Yake)

  

Du'aa Mbalimbali  Anazozihitaji Muislamu Kuzifahamu (Pamoja Na Matamshi Yake)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Du’aa Ya Kuona Mwezi Unapoandama [Miezi Yote Si Ramadhwaan Pekee]

اللهُ أَكْـبَر، اللّهُمَّ أَهِلَّـهُ عَلَيْـنا بِالأمْـنِ وَالإيمـان، والسَّلامَـةِ والإسْلامِ، وَالتَّـوْفيـقِ لِما تُحِـبُّ وَتَـرْضَـى، رَبُّنـا وَرَبُّكَ اللهُ.

Allaahu Akbar, Allaahumma Ahillahu ‘alaynaa bil-amni wal-iymaani, wassalamaati wal-Islaami, wattawfiyqi limaa Tuhibbu Rabbunaa wayardhwaa Rabbuna wa-Rabbuka-Allaah

 

Allaah ni Mkubwa, Ee Allaah, Uuanzishe kwetu kwa amani na imani, na usalama na Uislamu, na taufiqi ya kile Unachokipenda Mola wetu na kukiridhia, Mola  wetu na Mola wako ni Allaah

 

Du'aa Ya Kwenda Msikitini 

اللّهُـمَّ اجْعَـلْ فِي قَلْبـي نُوراً ، وَفي لِسَـانِي نُوراً،   وَفِي سَمْعِي نُوراً, وَفِي بَصَرِيِ نُوراً, وَمِنْ فََوْقِي نُوراً , وَ مِنْ تَحْتِي نُوراً, وَ عَنْ يَمِينيِ نُوراَ, وعَنْ شِمَالِي نُوراً, وَمْن أَماَمِي نُوراً, وَمِنْ خَلْفيِ نُوراَ, واجْعَلْ فِي نَفْسِي نُوراً, وأَعْظِمْ لِي نُوراً, وَعظِّمْ لِي نُوراً, وَاجْعَلْ لِي نُوراً, واجْعَلنِي نُوراً, أللَّهُمَّ أَعْطِنِي نُوراً, واجْعَلْ فِي عَصَبِي نُوراً, وَفِي لَحْمِي نُوراً, وَفِي دَمِي نُوراً وَفِي شَعْرِي نُوراً, وفِي بَشَرِي نُوراً (أَللَّهُمَّ اجِعَلْ لِي نُوراً فِي قّبْرِي  وَ نُوراَ فِي عِظاَمِي) (وَزِدْنِي نُوراً, وَزِدْنِي نُوراَ , وَزِدْنِي نُوراً) (وَهَبْ لِي نُوراً عَلَى نُوراً )

Allaahumma-j-'al Fiy Qalbiy Nuuraa,  Wa fiy Lisaaniy Nuuraa  Wa fiy Sam'iy Nuuraa, Wa Fiy Baswariy Nuuraa, Wa Min Fawqiy Nuuraa, Wa Min Tahtiy Nuuraa, Wa 'An Yamiiniy Nuuraa, Wa 'An Shimaliy Nuuraa, Wa Min Amaamiy Nuuraa, Wa Min Khalfiy Nuuraa, Waj-'al Fiy Nafsiy Nuuraa, Wa A'adhwim Liy Nuuraa, Wa 'Adhwim Liy Nuuraa, Waj-'al-Liy Nuuraa, Waj-alniy Nuuraa, Allaahuumma A'atwiniy Nuuraa, Waj'al fiy 'Aswabiy Nuuraa, Wa fiy Lahmiy Nuuraa, Wa fiy Damiy Nuuraa Wa fiy Sha'ariy Nuuraa, Wa fiy Bashariy Nuuraa. Allaahumma-j'al liy Nuuran  fiy Qabriy, Wa Nuuran Fiy 'Idhaamiy,   Wazidniy Nuuraa, Wazidniy Nuuraa, Wazidniy Nuuraa, Wahab liy Nuuran 'Alaa Nuuraa.

 

"Ee Allaah, Weka katika moyo wangu nuru, na katika ulimi wangu nuru, na katika masikio yangu nuru, na katika macho yangu nuru, na juu yangu nuru, na chini yangu nuru, na kuliani kwangu nuru, na kushotoni kwangu nuru, na mbele yangu nuru, na nyuma yangu nuru, na Weka katika nafsi yangu nuru, na Nifanyie kubwa nuru, na Nifanyie nyingi nuru, na Uniwekee mimi nuru, na Nifanyie mimi nuru, Ee Allaah  Nipe nuru, na Uweke  katika  mishipa yangu nuru, na katika  nyama  yangu nuru, na katika damu yangu nuru, na katika nywele zangu nuru, na katika ngozi yangu nuru, (Ee Allaah  Niwekee nuru katika kaburi langu, na nuru katika mifupa yangu) (Na Unizidishie nuru, na Unizidishie nuru, na Unizidishie nuru) (na Unipe nuru juu ya nuru )".

 

Du'aa Ya Kuingia Msikitini

أَعُوذ باللهِ العَظيـم وَبِوَجْهِـهِ الكَََرِِيـمِ وَسُلْطـانِهِ القََدِيـمِ مِنَ الشّيْـطانِ الرَّجِـيمِ،[ بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ] [وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله]، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِكَ

A'udhu BiLLahil-'Adhwiym Wabiwaj-hihi-l-Kariym Wasul-twaanihi-l-Qadiym Mina-shaytwaanir-rajiym.  BismiLLahi Was-Swalaatu Wassalaamu 'Alaa RasuliLLah.  Allaahummaf-tah liy Abwaaba Rahmatika.

 

"Najilinda na Allaah  Aliye Mtukufu, na kwa uso Wake, Mtakatifu, na kwa utawala Wake wa kale, kutokana na shetani aliyeepushwa na rehma za Allaah, (Kwa Jina la Allaah na rehma) (Na amani zimfikie Rasuli wa Allaah ) Ee Allaah  Nifungulie milango ya rehma Zako"

 

Du'aa Ya Kutoka Msikitini

بِسمِ الله وَالصّلاةُ وَالسّلامُ عَلَى رَسولِ الله، اللّهُـمَّ إِنّـي أَسْأَلُكَ مِـنْ فَضْـلِك، اللّهُـمَّ اَعْصِمْنـي مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجـيم

Bismillahi Was-Swalaatu Was-Salaamu 'Alaa RasuliLLah, Allaahumma Inniy As-aluka Min Fadhlika Allaahumma A'aswimniy Minash-shaytaani-rajiym. 

 

"Kwa Jina la Allaah na rehma na amani zimfikie Rasuli wa  Allaah, Ee Allaah  hakika mimi nakuomba katika fadhila Zako, Ee Allaah najilinda kutokana na shetani aliyeepushwa na rehma Zako (aliyelaaniwa )"

 

Du'aa Ya Qunuut Ya Witr

اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.

Allaahummah-diniy fiyman Hadayta , Wa 'Aafiniy fiyman 'Aafayta, Watawallaniy fiyman Tawallayta, Wabaarik liy fiymaa A'atwayta, Waqiniy Sharra Maa Qadhwayta, Fainnaka Taqdhwiy Walaa Yuq-dhwa 'Alayka, Innahu Laa yadhillu  mawwaalayta, Walaa Ya'izzu man 'Aadayta, Tabaarakta Rabbana Wa Ta'aalayta.

 

"Ee Allaah  Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afaya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya  wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi.  Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui) Umetakasika Ee Rabb wetu na Umetukuka".

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك

Allaahumma Inniy A'udhu Biridhwaaka Min Sakhatwika, Wabimu'aafaatika min 'Uquubatika, Wa A'udhu Bika Minka, Laa Uhswiy Thanaan 'Alayka, Anta Kamaa Ath-nayta 'Alaa Nafsika.

 

"Ee Allaah  hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda  Kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe"

اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك

Allaahumma Iyyaaka Na'abud Walaka Nuswalliy Wanasjudu, Wa-Ilayka Nas'aa Wanahfidu, Narju Rahmataka, Wanakhsha 'Adhaabaka, Inna 'Adhaabaka Bil-Kaafiriyna Mulhaqq.  Allaahumma  Innaa Nasta'iynuka Wanastaghfiruka, Wanuthniy 'Alaykal-khayra, Walaa Nakfuruka, Wanu-uminu Bika, Wanakhdhwa'u Laka, Wanakhla'u Man Yakfuruka.

 

"Ee Allaah, Wewe tu Ndiye tunaekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia.  Ee Allaah  hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru"

 

Du'aa baada ya salamu katika swalaah ya Witri (Mwisho kabisa baada ya kumaliza Swalaah yote na si kila baada ya Rakaa mbili au nne)  

سُـبْحانَ المَلِكِ القُدّوس

Subhaanal-Malikul-Qudduus

 

"Ametakasika Allaah  Mfalme, Mtakatifu"

(mara tatu)

(Kisha unavuta kwa sauti )

 ربِّ الملائكةِ والرّوح

Rabbul-Malaaikati War-Ruuh

 

"Ee Rabb wa Malaika na wa Jibriyl"

 

Du'aa Kabla Ya Kula

Anapotaka kula mmoja wenu chakula basi aseme:  

بِسْمِ الله

Bismillahi

 

"Kwa Jina La Allaah"

Na akisahau mwanzo wake basi aseme:

بِسْمِ اللهِ في أَوَّلِهِ وَآخِـرِهِ

Bismillahi Fiy Awwalihi Wa Aakihirihi

"Kwa jina la Allaah  mwanzo Wake na mwisho Wake"

 

Yeyote ambae Allaah Amemruzuku chakula aseme:

اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَأَطْـعِمْنا خَـيْراً مِنْـهُ

Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wa Atw'imna Khayran minhu.

"Ee Allaah Tubariki katika chakula hichi na Tulishe bora kuliko hichi "

Na yeyote ambae Amemruzuku maziwa basi aseme:

اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَزِدْنا مِنْهُ

Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wazidna  Minhu

"Ee Allaah Tubarikie kinywaji hichi na Utuzidishie"

 

Du'aa Ya Baada Ya Kula

الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلا قُوَّةٍ

Alhamduli-Llahi-lladhiy Atw'amaniy Haadhaa Warazaqaniyhi Min Ghayri Hawlim-Minniy Walaa Quwwatin.

 

"Sifa njema ni za Allaah  Ambaye Amenilisha mimi chakula hichi na Akaniruzuku pasina uwezo wangu wala nguvu zangu"

الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فيه، ]غَيْرَ مَكْفِيٍّ[ وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبُّـنا

AlhamduliLLahi Hamdan Kathiyran Twayyiban Mubaarakan Fiyhi, Ghayra Mukfiyyi  Walaa Muwadda'iw- Walaa Mustaghna 'Anhu Rabbunaa.

 

"Sifa njema ni za Allaah, sifa nyingi nzuri, zenye  baraka ndani yake, zisizo toshelezwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo mtu.  Ee Rabb wetu"

 

Du'aa Ya Mgeni Kumuombea Aliyemkaribisha Chakula

اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ

Allahumma Baarik Lahum Fiyma Razaq-tahum Waghfir-lahum War-ham-hum.

"Ee Allaah Wabariki katika Ulichowaruzuku na Uwasemehe na Uwarehemu" 

 

Du'aa Ya Kumuombea Aliyekupa Kinywaji Au Anayetaka Kukupa

اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي

Allaahumma Atw'im Man Atw'amaniy Wasqi Man Saqaaniy.

"Ee Allaah Mlishe aliyenilisha na Mnyweshe aliyeninywesha"

 

Du'aa ya kumuombea uliyefuturu/futari kwake

أَفْطَـرَ عِنْدَكُم الصّـائِمونَ وَأَكَلَ طَعامَـكُمُ الأبْـرار، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُ الملائِكَـة

Aftwara 'Indakumu-Swaaimuna Wa Akala Twa'aamakumul-Abraar, Waswallat 'Alyakumul-Malaaikah.

"Wafuturu kwenu waliofunga na wale chakula chenu watu wema, na wawaombee rehema malaika"

 

Du'aa Ya Aliyealikwa Chakula Lakini Akawa Amefunga

Akialikwa mmoja wenu aitike mwito, akiwa amefunga basi awaombee Du'aa na kama hakufunga basi ale

 

Anachosema Aliyetukanwa Hali Ya Kuwa Amefunga

إنِّي صَائِمٌ ,  إنِّي صَائِمٌ

Inniy Swaaimun Inniy Swaaimun

"Hakika mimi nimefunga, hakika mimi nimefunga"

 

 

 

 

Share