272-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 272: لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 272-Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾
272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii:
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ
“Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa…” imeteremka kuhusu Swahaba ambao walikuwa hawawapi msaada hata kidogo ndugu zao wa karibu katika Washirikina, basi hapo ikateremka:
الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾
Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara. (2:27) [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]