04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kulipa Ramadhwaan Au Siku Sita Za Shawwaal? Inafaa Kulipa Jumatatu Na Alkhamiys

Kulipa Ramadhwaan Au Siku Sita Za Shawwaal? Inafaa Kulipa Jumatatu Na Alkhamiys?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inafaa kufunga siku sita za Shawwaal kabla ya kulipa deni la Ramadhwaan? Na inaruhusiwa kulipa kwa kufunga siku za Jumatatu na Alkhamiys katika mwezi wa Shawwaal kwa niyyah ya kulipa deni na niyyah ya kupata thawabu za Swiyaam za Sunnah ya Jumatatu na Alkhamiys?

 

 

JIBU:

 

Thawabu za kufunga Sittatu Ash-Shawwaal hazipatikani ila baada ya kukamilisha mwezi wa Ramadhwaan. Kwa hiyo kama mtu ana deni la Ramadhawan basi kwanza alipe deni kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal, kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

مَنْ صَامَ رَمَضَانَ ثُمَّ أَتْبَعَهُ سِتًّا مِنْ شَوَّالٍ كَانَ كَصِيَامِ الدَّهْرِ  

((Atakayefunga Ramadhwaan, kisha akafuatia na Sitta za Shawwaal Swiyaam zake zitakuwa kama ni Swiyaam za mwaka)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Ad-Daarimiy].

 

Kutokana na Hadiyth  hiyo tunasema kwamba, yeyote mwenye deni la Swawm ya Ramadhwaan alipe kwanza kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal. Na ikiwa Siku Sita za Shawwaal zimeangukia siku ya Jumatatu na Alkhamiys atapata thawabu zote (thawabu za Swiyaam ya Siku Sita Za Shawwaal na thawabu za Swiyaam ya Jumatatu na Alkhamiys) kwa niyyah hizo kutokana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

(إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى ))

((Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia))

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fiqhul Ibaadaah, ukurasa 222, Maktabatul Iymaan]

 

 

 

Share