Mikate Ya Naan Ya Tui La Nazi Na yai

Mikate Ya Naan Ya Tui La Nazi Na yai

Vipimo

 

Unga vikombe 3 – chunga

Hamira kijiko cha supu 1

Yai 1

Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya supu

Tui la nazi   65 ml = 2 oz = ¼ cup

Sukari kijiko 1 cha chai

Maji ya vuguvugu kiasi ya kukandia

Chumvi kijiko 1 cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Katika bakuli, changanya unga, sukari, chumvi, hamira.
  2. Tia mafuta na nazi vuruga mpaka uchanganyike vizuri.
  3. Changanya yai, tia maji kiasi ya kukandia kama unga wa chapatti uwe laini.
  4. Funika uumuke, kisha katakata madonge
  5. Sukuma kiasi ya unene wa cm 2, weka tena uumuke kisha choma kwenye grill au timia wavu choma katika mkaa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

Share