Skip to main content

Fataawaa: Swalaah Ya 'Iyd Na Siku Ya 'Iyd09-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ikiwa Mtu Itampita Kitu Katika Takbiyrah Za ‘Iyd

Ikiwa Mtu Itampita Kitu Katika Takbiyrah Za ‘Iyd

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

"Yatamuondokea (hayatompasa) yale yaliyompita, na hivyo hivyo kama vile akisahau au mpaka akafikia kusoma (Suwrah) basi haleti tena (harudii tena), kwa sababu Sunnah imepita mahali pake Lakini ikiwa imempita pamoja na Imaam Rakaa kamili basi inabidi alete Takbiyrah za Rakaa hiyo iliyompita.

[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/241)]