Ukumbusho Wa Kukithirisha Swawm Mwezi wa Al-Muharram Na Swiyaam Ya Taasu'aa na 'Aashuraa (9 na 10 Al-Muharram) Pamoja Na Masiku Mengineyo
Al-Muharram
Ukumbusho Wa Kukithirisha Swiyaam (Funga) Za Mwezi wa Al-Muharram
Na Swiyaam Ya Taasu'aa na 'Aashuraa (9 na 10 - Al-Muharram) Pamoja Na Masiku Mengineyo
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ رواه مسلم
"Swiyaam (funga) bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni swawm ya mwezi wa Allaah wa Al-Muharram." [Muslim]
Tunawanasihi hali kadhalika kufunga siku ya Taasu'aa na 'Aashuraa (Tarehe 9 na 10 Al-Muharram) Asiyeweza Swawm tarehe 9 Al-Muharram basi baadhi ya 'Ulamaa wanasema kuwa mtu anaweza kufunga tarehe 10 na 11 Al-Muharram japokuwa hakuna Hadiyth sahihi ya kufunga siku ya baada yake; yaani Muharram 11. Na asiyejaaliwa kuunganisha Swawm tarehe 9 pamoja na tarehe 10 au kuunganisha Swawm tarehe 10 pamoja na 11 Al-Muharram, basi asikose Swawm ya tarehe 10 Al-Muharram pekee. Hayo ni kutokana na fadhila zake za kufutiwa madhambi ya mwaka mmoja kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((صِيَامُ يَوم عاشوراء إنِّي أحْتَسبُ علَى اللهِ أن يُكفِّرَ السَّنةَ التِي قبلَه)) رواه مسلم
"Swawm ya siku ya 'Ashuraa, nategemea kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia." [Muslim]
Kwa faida zaidi soma makala katika kiungo kifuatacho:
Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharam Na Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake
Masiku mengineyo ya Swiyaam za Sunnah na fadhila zake:
Jumatatu na Alkhamiys:
عن أبي هريرة رضي الله عنه: تُعرَضُ الأعمالُ يومَ الاثنينِ والخميسِ فأحبُّ أن يُعرَضَ عملي وأنا صائمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “'Amali zinapandishwa siku ya Jumatatu na Alkhamiys, basi napenda kwamba zipandishwe 'amali zangu nikiwa mimi niko katika Swawm.” [Swahiyh At-Tirmidhiy 747, Swahiyh At-Targhiyb 1041]
Swiyaam ya Jumatatu:
عَنْ أَبِي قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الِاثْنَيْنِ فَقَالَ: (( فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ)) .
Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Swawm ya Jumatatu akasema: “Nimezaliwa siku hiyo na siku hiyo nimeteremshiwa (Qur-aan).” [Muslim]
Ayyaamul-Biydhw (Tarehe 13, 14, 15)
Swawm Ya Nabiy Daawuwd: Siku Kufunga Na Siku Kuacha kutokana na Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
أَحَبُّ الصِّيَامِ إِلَى اللَّهِ صِيَامُ دَاوُدَ، كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا
"Swawm inayopendeza zaidi kwa Allaah ni Swawm ya Daawuwd, alikuwa anafunga siku moja na anakula siku moja” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida za fadhila za Swiyaam:
Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah
Tutaweka taarifa za kuandama mwezi In Shaa Allaah.