Faida Na Hukmu Za Kuomba Tawbah - 01

 

Faida Na Hukmu Za Kuomba Tawbah - 01

 

Alhidaaya.com

 

 

Faida ya kuomba Tawbah si tu kughufuriwa madhambi yote Muislamu akajihisi kuwa basi inamtosheleza kuwa hana dhambi tena, hapana si hiyo tu! Bali pia kuna faida nyingi sana zaidi ya hiyo zinazomrudia mwenyewe mja anayeomba tawbah na ambazo bila shaka kila mtu angelipenda sana kuzipata faida hizo. Miongoni mwa faida hizo ni: 

 

1-Kujaaliwa Kupata Starehe Na Fadhila Kutoka Kwa Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa: 

 

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ﴿٣﴾

Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa; na Atampa kila mwenye fadhila, fadhila Zake. Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakhofu adhabu dhidi yenu ya Siku kubwa.” [Huwd:3]

 

2-Kuletewa Neema ya Mvua Na Kuzidishiwa Nguvu: 

 

 وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ﴿٥٢﴾

“Na enyi kaumu yangu!  Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni (kutoka) mbinguni mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wahalifu.” [Huwd:52]

 

3-Mbali Ya Mvua Bali Na Kujaaliwa Mali Na Watoto, Na Kupewa  Kila Aina Ya Neema:

 

Nuwh ('Alayhis-salaam) alipowalingania watu wake miaka kuwatoa katika shirki, aliwanasihi waombe maghfirah na tawbah na akawatajia fadhila na faida zake: 

 

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria. Atakutumieni mvua tele ya kuendelea. Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh:10-12]

 

4- Kujaaliwa Jannah Ya Milele  

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema). [Aal-‘Imraan:135-136]

 

 

Inaendelea in Shaa Allaah...

 

Share