Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kwanini Dini ya Kiislamu imeitwa Islaam?

Kwanini Dini Ya Kiislamu Imeitwa Islaam?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Kwanini Dini ya Kiislamu imeitwa Islaam?

 

 

JIBU:

 

Kwa sababu anayeingia katika Uislamu anajisalimisha (aslama) kwa Allaah na (istaslama) anasalimu amri kwa yale yote yanayotoka kwa Allaah na kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hukmu (shariy’ah); Anasema Ta’aalaa:

 

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ

130. Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? [Al-Baqarah: 130]

 

Mpaka kauli Yake:

إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾

131. Rabb wake Alipomwambia: “Jisalimishe na utii” (Ibraahiym) Akasema: “Nimejisalimisha na kutii kwa Rabb wa walimwengu.” [Al-Baqarah: 131]

 

Na Anasema:

 

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ  

112. Ndio! Bali yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali yeye ni mwenye kufanya ihsaan basi atapata ujira wake kwa Rabb wake. [Al-Baqarah: 112]

 

 

[Fataawaa Islaamiyyah (8/355)]

 

 

Share