Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuweka Wasiya Kuzikwa Msikitini Kwa Kuwa Amejenga Yeye Msikiti

 

Kuweka Wasiya Kuzikwa Msikitini Kwa Kuwa Amejenga Yeye Msikiti

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Niini hukmu ya mtu aliyejenga Masjid kisha akaweka wasia kuwa azikwe humo? Kisha akazikwa sasa nini la kufanya?

 

 

JIBU:

 

Wasia huo wa kuzikwa katika Masjid (Msikiti) haufai. Kwa sababu Masjid si mahali pa makaburi. Na hairuhusiwi kuzikwa katika Masjid. Na kutimiza ombi hilo la wasiya ni haramu.

 

Na lilowajibika sasa ni  kufukua kaburi na kuhamisha maiti katika eneo la makaburi ya Waislamu.

 

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Ar-Rasaail (2/292)]

 

 

Share