04-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayeshuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah… Allaah Atamuingiza Jannah Kwa ‘Amali Alizonazo

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

04-Atakayeshuhudia Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah … Allaah Atamuingiza Jannah Kwa ‘Amali Zozote Alizonazo:

 

 

عن عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رضي الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah Bin Swaamit (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeshuhudia kwa kuamini na kukiri moyoni kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)) [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)].

Share