Imaam Ibn Baaz: Talaka Ya Mjamzito

Talaka Ya Mjamzito

 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa ikiwa mwanamke anaweza kupewa talaka wakati akiwa mjamzito.

 

 

 

JIBU:

 

Alisema:

 

Huu ni ufahamu uliozoeleka miongoni mwa baadhi ya watu.

 

Baadhi ya watu wanadhani ya kuwa mwanamke mjamzito hawezi kupewa talaka.

 

Sijafahamu wapi wametoa haya maelezo, maelezo haya hayana asili kutoka kwa 'Ulamaa.

Bali mtazamo wa  'Ulamaa wote ni kwamba; mwanamke mjamzito anaweza kupewa talaka.

 

'Ulamaa wamekubaliana katika jambo hili, Na hakuna ikhtilaaf. Talaka kulingana na Sunnah inamaanisha kuwa mwanamke anaweza kuachika katika hali mbili:

 

1. Anaweza kuachika wakati ni mjamzito; hii ni talaka ya Sunnah na si talaka ya bid'ah.

 

2. Anatakiwa kuwa twahara (si katika masiku yake ya hedhi) na mume wake ikiwa hajamgusa (hajafanya naye tendo la ndoa), anatakiwa awe ni twahara kutokana na hedhi au nifaas (damu ya uzazi) na kabla hajafanya naye tendo la ndoa.

 

Talaka hii ni kwa mujibu wa (talaka za) Sunnah.

 

 

[Fataawa Atw-Taalaaq, mj. 1, uk. 45-46]

 

 

Share