06-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Abashiriwe Jannah Mwenye Kushuhudia Akiwa Na Yakini Moyoni Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah.

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

06-Abashiriwe Jannah Mwenye Kushuhudia Akiwa Na Yakini Moyoni

Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah.

 

 

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita:

 

((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)) [Muslim]

 

 

 

 

 

 

 

 

Share