Skip to main content

Swalaah Za Sunnah Zilizo Sahihi Na Ambazo Si Sahihi

 Swalaah Za Sunnah Zilizo Sahihi Na Ambazo Si Sahihi

www.alhidaaya.com

SWALI:

Assalaamualaykum ndugu zangu,

Mimi siku zote naamka saa nane  za usiku,  yaani na amshwa naturally. Nina sali kwa mpango ufuatao:

1. Sunnatil-udhuu rakaa 2

2. Sunnati Rasulu-Allaah Swalla Allaahu alayhi wa sallam wa sallam rakaa 2

3. Sunnat tahajjud rakaa 2

4. Sunna ya usiku ule  raka ....kama ilvyoandikwa

5. Sunnat hajjat rakaa  2, 2,2,  mujibu wa haja  zangu.  

6. Sunnat tawba rakaa  2

7. Salaatul  witr rakaa 3.

By the time nimewahi  zote Swalah ya fajr ni tayari.  na endelea  kufanya  dhikruAllaah  baada ya swalah  ya fajr mpaka time ya ishraaq na tena naendelea kuwepo  kwenye  msala kwa dhikru-Allaah mpaka swalah ya dhuhaa.

Je nifafanulieni wapi nimekosea na  nifanye sahihi namna gani

Jazaakallahukheir

Fiamaanillah

JIBU:

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Hakika ‘ibaadah ni jambo muhimu sana kwa kila Muislamu kwani katika kufanya ‘ibaadah yoyote ikiwa ya vitendo au kauli,  lazima masharti mawili yapatikane ndipo ‘ibaadah hiyo ikubaliwe nayo ni:

1-Ikhlaas – Iwe kwa kutaka Radhi za  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  na sio yenye Riyaa (kujionyesha) au sio yenye kutendeka kwa ajili ya maslahi ya kidunia.

2-Iwe inafanyika kutokana na mafunzo ya  Qur-aan na Sunnah.  

Tunakutajia hapa zilizo sahihi na zisizo sahihi kutokana na maelezo yako:

Swalaah

Daraja yake

Dalili/Maelezo

Sunnatul- Wudhuu  Rakaa mbili 

Sahihi

Bilaal (Radhwiya Allahu 'anhu) akiswali hata Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaota nyao zake ziko Jannah (Peponi) kwa kufanya hivyo

Sunnatul-Rasulu-Allaah

Sio sahihi

Hakuna dalili yoyote.

Tahajjud Rakaa 2

Sahihi

 Ni Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku) Unaweza kuswali mbili, au nne, au sita au nane ukamalizia na tatu za Witr

Sunnah ya usiku

Sahih

Nayo ni Qiyaamul-Layl. Ni Swalaah yoyote unayoswali baada ya ‘Ishaa kama ni kisimamo cha usiku.

Sunnah ya Haja

Haifai

Imepingwa na ‘Ulamaa kuwa ni Hadiyth dhaifu. Muislamu anaomba haja zake kwa kuomba du'aa kama kawaida.

Sunnati Tawbah

Sahihi

Anapofanya mja dhambi anaswali Rakaa mbili kuomba maghfirah

Salaatul Witr

Sahihi

Rakaa 3 unamalizia baada ya kuswali 8 au chini yake za Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku)

Hii imesisitizwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Unavyomalizia kuwa inafika Alfajiri kisha unaendelea kufanya Dhikru-Allaah hadi litoke jua kisha unaswali Swalaah ya Dhwuhaa, hakika Hadiyth hiyo baadhi ya ‘Ulamaa wameona kuwa ni dhaifu na wengineo wameona kuwa ni sahihi. Nayo inatokana na Hadiyth ifuatayo:

عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال : من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله  حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة  أخرج الترمذي  صححه الألباني

Imetoka kwa Anas kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jamaa'ah kisha akakaa Anamdhukuru Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhy na kaisahihisha Al-Albaaniy] 

Kwa hiyo tekeleza ambazo ni sahihi na epukana na ambazo si sahihi au zina utata.

Na Allaah Anajua zaidi