15-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Kutamka Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Miongoni Mwa Swadaqah

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

15-Kutamka Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Miongoni Mwa Swadaqah

 

 

عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه:  أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ  بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ: ((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Watu katika Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ee Rasuli wa Allaah! Watu wenye mali wameondoka na thawabu nyingi; wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga na wanatoa swadaqah kwa fadhila za mali zao. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani Allaah Hakukujaalieni njia ya kutolea swadaqah? Hakika kila (kutamka) Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah. Na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah. Na kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah, na kila Tahliyl (Laa ilaaha illa Allaah) ni swadaqah. Na kuamarisha mema ni swadaqah. Na kukataza munkari ni swadaqah. Na mmoja wenu kujimai (na mkewe) ni swadaqah.”  Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah. Hivi mmoja wetu kujitoshelezea kwa shahawa yake atakuwa anapata thawabu? Akasema: “Mnaonaje kama atajitosheleza kwa njia ya haraam angelipata dhambi? Hivyo basi ikiwa atafanya kwa njia ya halaal, atapata thawabu.”  [Muslim]

 

 

Share