20-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayeamka Usingizi Akasema: “laa ilaaha illa Allaah…” Atataqabaliwa Du’aa Na Swalaah Yake.

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com 

 

20-Atakayeamka Usingizi Akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu…” Atataqabaliwa

Du’aa Na Swalaah Yake.

 

 

 عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ  وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ. ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي  أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ, فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))

 

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah” (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema: “Rabbigh-fir-liy” [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)). [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 

Share