Skip to main content

Saladi Ya Quinoa Na Parachichi

Saladi

Saladi Ya Quinoa Na Parachichi  

Vipimo

Quinoa – vikombe 2

Parachichi  (Avocado) – 1

Pilipili boga jekundu – 1

Sosi ya saladi (salad dressing)

Mafuta ya zaytuni – ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Roweka kidogo quinoa kisha chemsha kidogo tu  kisha chuja maji na kamua.

  1. Kisha weka katika bakuli.
  2. Katakata parachichi, pilipili boga, weke uchanganye pamoja na quinoa ikiwa tayari kuchanganywa na dressing yake.

Sosi (Dressing ya saladi)

Changanya mafuta ya zaytuni, chumvi, ndimu ikiwa tayari kumiminwa na kuchanganwa na saladi

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)