Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ramadhwaan: Ikiwa Ana Majukumu Lipi Bora Atekeleze I’tikaaf Majukumu Yake?

Ikiwa Ana Majukumu Je Lipi Bora Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

1. Ikiwa mtu ana majukmu ya ahli zake na ikiwa amewajibika nayo, basi ni waajib kwake kuyatimiza na hivyo basi, kutekeleza I’tikaaf huwa ni dhambi kwake.

 

2. Na ikiwa si yenye kuwajibika kwake, basi hata hivyo kuyatimiza huwa ni bora kwake kuliko I’tikaaf.

 

3. Ama mtu aliyekuwa huru, basi I’tikaaf inakuwa ni haki kwake ki-shariy’ah. Lakini ikiwa ana majukumu katika makumi ya mwanzo, lakini kisha akawa huru kisha akataka kutekeleza I’tikaaf masiku yaliyobakia basi hakuna neno.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]

 

 

Share