41-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Du’aa Ya Kumwogopa Mtawala Na Kukhofu Kushambuliwa: Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa

 

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

41-Du’aa Ya Kumwogopa Mtawala Na Kukhofu Kushambuliwa: Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa

 

عنِ ابنِ عبَّاسٍ قالَ إذا أتيتَ سلطانًا مَهيبًا تخافُ أن يسطوَ بِكَ فقلِ

 

Athar ya Ibn ’Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) ambaye amesema: Utakapokwenda kwa mtawala anayetisha ambaye utakhofia kuwa atakushambulia, basi sema:

 

الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ

 

Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kunliy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3]

 

Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu Ambaye  Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja  (fulani - mtaje mtu unayemhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu.  Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka sifa Zako na Umeheshimika ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako.  

[Al-Bukhaariy - Adabul-Mufrad [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546], Swahiyh At-Targhiyb (2238)].

 

 

Share