Imaam Ibn Taymiyyah: Maulidi: Ingelikuwa Maulidi Ni Thawabu Swahaba Wangekuwa Na Haki Zaidi

 

 

Ingelikuwa Maulidi Ni Thawabu Swahaba Wangekuwa Na Haki Zaidi Kututangulia

 

 

Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: “Baadhi ya watu, kwa kuwaiga Manasara wanafanya kwa kudai mazazi ya ‘Iysaa (‘Alayhis salaam), au kwa sababu ya mapenzi yao kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kupenda kwao kumtukuza, wanasherehekea mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Japokuwa kuna utata mkubwa baina ya wanachuoni kuhusu tarehe hasa aliyozaliwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Waislamu wa mwanzo hawakufanya hilo, japokuwa kulikuwa na sababu nzuri kumheshimu na kuyaonyesha mapenzi yao kwake na hakukuwa na kikwazo chochote katika kufanya hilo.

 

Hivyo, lau kusherehekea mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yalikuwa ni jambo la thawabu na zuri wangekuwa na haki zaidi ya kututangulia katika hilo, kwani yale mapenzi yao na heshima yao kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yalikuwa ni makubwa kuliko yetu. Na pia walikuwa na hamu zaidi ya kutekeleza matendo mema kiujumla kuliko sisi.”  

 

[Iqtidhwaa’ asw-Swiraatwal Mustaqiym Mukhaalafatu Aswhaabul Jahiym, Mj. 2, uk. 619 na Majmuu‘ al-Fataawaa, Mj. 1, uk. 312]

 

 

 

Share