12-Zawadi Kwa Wanandoa: Yachukizayo Kwenye Sherehe ya Harusi

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

12- Yachukizayo Kwenye Sherehe ya Harusi

 

منكرات الأفراح

 

 

 

 

Katika jumla ya mambo yenye kuchukiza katika sherehe ya ndoa ni

 

  • Kuzidi kwa ala za muziki, na nyimbo mbaya chafu za matusi zenye kuchochea hisia za chuki na ngono zenye kuimbwa na watu waliobobea katika maasia. Kisha kibaya zaidi ni ule mchanganyiko wa wanawake na wanaume ambalo ni jambo lisilo la lazima kabisa katika sherehe na haswa zaidi za harusi. Kadhalika kuingia kwa wapiga picha na wapiga ngoma na wachezaji wake kwa Bwana na Bibi harusi na kuwaona wanawake na fitna (mapambo yao) zao na kudhihirika uchi wao mbele yao, hivyo basi kupelekea kudhihiri kwa makosa katika mazingira yaliyotawaliwa na shetani.

 

  • Na katika jumla ya machukizo ni upigaji wa honi za magari na mazumari mabarabarani, jambo lenye kusababisha kuamsha na kuwastua waliolala, wagonjwa na wanafunzi waliopo madarasani.

 

  • Na mengine yenye kuingia katika machukizo ni ile ada chafu na mbaya ya kujifakharisha baina ya watu iliyopo katika baadhi za sehemu, kwa mfano mmoja wao kusema: Shabbash kwa Fulani, na anaanza kutaja mali alizotoa katika kuchangia harusi, na anatokezea mwingine anayehamasika na anatoa zaidi ya yule wa mwanzo kwa lengo la kujifakharisha na kujitukuza na kujiona mbele za watu.

 

  • Na katika yasiyopendeza ni kuingia kwa Bwana harusi ndani kwa Bibi harusi na kukaa nae pembeni, katikati, ya wanawake wasiojisitiri, wenye kujionesha, na haingii peke yake bali ataingia na nduguze wengine.

 

  • Na mengineyo katika hayo ni ulipuaji wa fataki na baruti eti kudhihirisha furaha yao na kuonekana washiriki wazuri wa harusi ile. Huu ni ujahili na upotefu, je, ni Mabwana harusi wangapi na Mabibi harusi wangapi ambao harusi zao ziligeuka kuwa ni khitma kwa hayo na Mabwana harusi wengine kuingizwa jela na si kuingia kwa mkewe!!.

 

  • Hali kadhalika mandhari ya sherehe yanapoonyesha ufakhari na kujiona na israfu na kujikalifu kwa taklifa zisizokuwa za msingi na ambazo anagharimika kwazo Bwana harusi kwa taabu ni katika mambo yenye kuchukiza katika sherehe za harusi.

 

  • Uvaaji wa kupita mipaka kwa wanawake kwenye sherehe za harusi na utengenezaji wa nywele na kujifananiza na wasiokuwa Waislamu, yote haya yanagharimu fedha nyingi sana mbali na uchafu unaoenezwa na fitna za hali hizi.

 

 

Share