008-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Najsi Zinazosamehewa
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Twahara
008-Najsi Zinazosamehewa
Kuna kauli mbalimbali za Maulamaa kuhusu aina na kiasi cha najsi ambayo inaweza kuingia katika nguo, au mahala, au mwilini na inakuwa ni yenye kusamehewa. Isipokuwa kidhibiti cha najsi zinazosamehewa ni udharura, kuenea kwa wingi, kuwa ni vigumu kujikinga nayo, na kuwepo tabu na uzito mkubwa katika kuiondosha. [Al-Fiqh Al-Islaamiy wa Adillatuhu (169 – 177)].