Fadhila Za Qur-aan Na Umuhimu Wake: Aayaat Za Qur-aan

 

Fadhila Za Qur-aan  Na Umuhimu Wake: Aayaat Za Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

1-Qur-aan imejaa Baraka za Allaah ('Azza wa Jalla).

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ

Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale ambayo yaliyokitangulia  [Al-An’aam: 92]

 

Na pia kauli Yake Allaah ('Azza wa Jalla):

 

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili. [Swaad: 29]

 

 

 

2-Qur-aan imejaa hikma:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu chenye hikmah. [Yuwnus: 1]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يس ﴿١﴾

Yaa Siyn.

 

وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾

Naapa kwa Qur-aan yenye hikmah. [Yaasiyn: 1-2]

 

 

 

3-Qur-aan ni Shifaa (Poza) na Rahmah kwa Waumini.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾

Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rahmah kwa Waumini; na wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa khasara. [Al-Israa: 82]

 

Ili kuipata Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), Muislamu unapaswa kuisikiliza kwa makini pindi inaposomwa Qur-aan kama Anavyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A’raaf: 204]

 

 

 

4-Qur-aan inazidisha Iymaan kwa Waumini na isisimua ngozi na inalainisha nyoyo na inazidi kuongoza: 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa. [Az-Zumar: 23]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٢﴾

Hakika Waumini ni wale ambao Anapotajwa Allaah, nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia iymaan, na kwa Rabb wao wanatawakali. [Al-Anfaal: 2]

 

 

 

5-Qur-aani ni Nuru (mwangaza) na inamtoa mtu kutoka kizani kuingia katika Nuru, akiwa ni Muislamu au kafiri:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾

Enyi watu!  Kwa yakini imekujieni burhani kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana. [An-Nisaa: 174] 

 

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwatoe watu kutoka kwenye viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Rabb wao, waelekee katika njia ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Ibraahiym: 1]

 

  

6-Qur-aan Inaongoza katika yaliyonyooka na inabashiria ujira mkubwa kabisa.  

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ﴿٩﴾

Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa. [Al-Israa: 9]

 

 

Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

 

طس ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْقُرْآنِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿١﴾

Twaa Siyn. Hizo ni Aayaat za Qur –aan na Kitabu kilicho bayana.

 

هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾

Mwongozo na bishara kwa Waumini.  [An-Naml: 1-2]

 

 

 

7-Qur-aan ni mawaidha ya Waumini na pia ni Shifaa (Poza) na Rahmah, na mwongozo  na pia ni bora kuliko yote yaliyomo duniani:

 

Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾

Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rahmah kwa Waumini.

 

 

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾

 Sema: “Kwa fadhila za Allaah na kwa rahmah Yake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni khayr kuliko wanayoyakusanya. [Yuwnus: 57-58]

 

 

 

8-Qur-aan  ni mwongozo na ni pambanuo linalobainisha na kutenganisha haki na batili:

 

 

Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ  

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 185]
 

 

Pambanuo hilo la kubainisha haki na batili ni kwa ajili ya kuwaonya walimwengu wote, Waislamu na makafiri. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Fuqaan: 1]

 

 

 

9-Kusoma Qur-aan ni kujichumua thawabu tele mfano wa biashara isiyokhasirika na juu ya hivyo ni kupata ujira na fadhila za Allaah ('Azza wa Jalla):

 

Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea.

 

لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾

Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir: 29-30]

 

 

 

10-Hawako sawa wanaosoma Maneno ya Allaah na wasiosoma:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya khayr, na hao ni miongoni mwa Swalihina. [Aal-‘Imraan: 114]

 

 

 

11-Qur-aan ni uhai wa nyoyo za wana Aadam, kinyume chake ni kama moyo uliokufa!

 

Mfano wa nyoyo zilokufa ni kama za waliokuwa makafiri kisha wakaingia Uislamu nyoyo zao zikahuika:

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ

Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo? [Al-An’aam]

 

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameita Qur-aan kuwa ni Ruwh (uhai) inaongoza katika njia iliyonyooka:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. [Ash-Shuwraa: 52]

 

 

 

12-Wanaohifadhi Qur-aan wanasifiwa kuwa ni wenye ilmu kwa kuhifadhi Aayat za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika nyoyo zao.

 

Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ  

Bali hizo ni Aayaat bayana (zimehifadhika) katika vifua vya wale waliopewa elimu.  [Ar-Ruwm: 49]

 

 

13-Wenye kushikamana na Qur-aan watapata ujira adhimu:

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٧٠﴾

Na wale wanaoshikilia imara Kitabu na wakasimamisha Swalaah, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa watendao mema. [Al-A’raaf: 170]

 

 

 

14-Qur-aan Haina dosari wala ubatilifu wala haina shaka.

 

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ﴿٤١﴾

Hakika wale waliokanusha Ukumbusho ulipowajia (wataangamia). Na hakika hicho ni Kitabu chenye utukufu na udhibiti.

 

 

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾

Hakitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Fusw-Swilat: 41-42]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 الم ﴿١﴾

Alif Laam Miym.

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa [Al-Baqarah: 1-2]

 

 

 

15-Qur-aan ni Kalaamu-Allaah! (Maneno ya Allaah) Basi vipi mja usipende kuyasoma Maneno ya Muumba wako?

 

Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ﴿٦﴾

Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan), kisha mfikishe mahali pake pa amani. Hivyo kwa kuwa wao ni watu wasiojua. [At-Tawbah: 6]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا ﴿١٠٩﴾

 Sema: “Kama bahari ingelikuwa ni wino wa (kuandika) maneno ya Rabb wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Rabb wangu, japokuwa Tungelileta mfano wake kujaza tena.” [Al-Kahf: 109]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٧﴾

Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingekuwa ni kalamu, na bahari (ikafanywa wino), ikaongezewa juu yake bahari saba; yasingelimalizika Maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Luqmaan: 27]

 

 

 

16-Qur-aan inayosomwa katika Swalaah ya Alfajiri kwa sauti inashuhudiwa na Malaika.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾

Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa. [Al-Israa: 78]

 

 

 

17-Majabali na milima ingenyenyekea pindi Qur-aan ingeliteremshwa juu yake kwa kumkhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), seuze wewe ndugu Muislamu? 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 
لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۚ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢١﴾

 

Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya jabali, ungeliliona linanyenyekea likipasukapasuka kutokana na khofu ya Allaah. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu ili wapate kutafakari. [Al-Hashr: 21]

 

 

18-Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anashuhudia unapoisoma Qur-aan:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦١﴾

Na hushughuliki katika jambo lolote, na wala husomi humo katika Qur-aan, na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Rabb wako hata cha uzito wa chembe (au sisimizi) katika ardhi wala mbinguni na wala kidogo kuliko hicho na wala kikubwa zaidi ya hicho isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho bayana. [Yuwnus: 61]

 

 

19-Haiwezekani kamwe kuileta mfano wa Quraan hata kama watakusanyika walimwengu wote pamoja na majini! 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

 Sema: “Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” [Al-Israa: 88]

 

 

Haiwezekani hata kuleta Suwrah moja wala Aayah ya Qur-aan: 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri. [Al-Baqarah: 23-24]

 

 

Na Anasema pia Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾

Je, wanasema” “Ameitunga (hii Qur-aan)?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.” [Huwd: 13]

 

Hizo ni baadhi ya fadhila za Qur-aan na umuhimu wake kama zilivyotajwa ndani ya Qur-aan. Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida ziada:

 

 

Maamrisho Ya Kuisoma Qur-aan Na Kuifanyia Kazi

 

Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Katika Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Ni juu yako Muislamu kutilia hima kuisoma Qur-aan na  ikiwezekana uweze kuihifadhi na kuifanyia kazi ili ujichumie thawabu tele tele kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah.

 

 

 

 

 

 

 

 

Share