Skip to main content

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلطَّهَارَةِ - Kitabu Cha Twahara040-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Msafiri Akipukusa Kisha Akawasili Mjini Kwake

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

Mlango Wa Twahara

040-Msafiri Akipukusa Kisha Akawasili Mjini Kwake

Alhidaaya.com

Ikiwa msafiri atapukusa juu ya khufu zake siku moja na usiku wake au zaidi kisha akawasili kwake, ni lazima azivue khufu zake, aoshe miguu yake anapotawadha, kisha atakuwa na hali ile ile ya mkazi.

Na ikiwa msafiri amepukusa kwa muda wa chini ya siku na usiku wake, basi inajuzu kwake anapowasili mjini akamilishe muda uliosalia wa siku moja na usiku wake, kisha ni lazima azivue. 

Ibn Al-Mundhir amenukulu Ijma’a ya kila Mwanachuoni anayezungumzia kwa kuainisha kuhusu muda wa kupukusa. [Al-Awsatw (1/446)].