06-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Halaal Imebainika Na Haraam Imebainika

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 6

 

إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ

 

Hakika Halaal Imebainika Na Haraam Imebainika

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:  ((إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))  رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu  ‘Abdillaah An-Nu’umaan bin  Bashiyr  (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika halaal imebainika na haraam imebainika na baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haraam. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo (mpaka mwingine wa watu). Zindukeni!  Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haraam Alizoziharamisha. Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu cha nyama, kinapokuwa salama, mwili wote unakuwa salama. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share