Skip to main content

02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلصَّلَاةِ - Kitabu Cha Swalaah009-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swalaah: Adhana Na Iqaamah

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

Mlango Wa Swalaah

009-Adhana Na Iqaamah

Alhidaaya.com

Taarifu:

[Al-Lisaan, Al-Miswbaahul Muniyr, Sharhu Muntahaa Al-Iraadaat (1/122) na Al-Mumti’i (35-36)]

Maana ya adhana kilugha ni kutangaza. Allaah Anasema:

((وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ))

((Na tangaza kwa watu Hajj)) [Al-Hajji (27:22)]

Ama kisharia, ni kutaabudia kwa Allaah Mtukufu kwa kutangazia kuingia wakati wa Swalaah kwa utajo maalumu.

Iqaamah kilugha, ni kisoukomo cha kitenzi ((أقام)) kutokana na sentensi ya  أقام الشيء , anapokinyoosha mtu kitu kikanyooka. Pia neno hili lina maana nyinginezo kama kutulia, kudhihirisha na kuita. Ama kishariah, ni kutaabudia kwa Allaah kwa ajili ya kusimama na kuswali kwa utajo maalumu.