13-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Waumini Wanapaswa Kumpenda Kuliko Nafsi Zao

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

13-Waumini Wanapaswa Kumpenda Kuliko Nafsi Zao

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ  

Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.  [Al-Ahzaab: 6]

 

Na katika Hadiyth inayohusiana na kauli hiyo ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏ ((مَا مِنْ مُؤْمِنٍ إِلاَّ وَأَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِهِ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ‏: ((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ‏)) فَأَيُّمَا مُؤْمِنٍ تَرَكَ مَالاً فَلْيَرِثْهُ عَصَبَتُهُ مَنْ كَانُوا، فَإِنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضِيَاعًا فَلْيَأْتِنِي وَأَنَا مَوْلاَهُ))  البخاري   

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muumini yeyote isipokuwa mimi nina haki zaidi kwake (ya kupendwa na kutiiwa) kuliko watu wote duniani na Aakhirah. Someni mkipenda:

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ  

Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.  [Al-Ahzaab: 6]

 

Na Muumini yeyote aliyeacha mali basi na warithi jamaa zake. Na ikiwa ameacha deni  au Watoto masikini, basi na waje kwangu (niwalipie madeni yao na niwahudumie) mimi ni mlinzi wao.  [Al-Bukhaariy]     

 

Na Hadiyth nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عبد اللَّهِ بْنَ هِشَامٍ قَالَ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ آخِذٌ بِيَدِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ لَهُ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ إِلاَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ نَفْسِكَ)) فَقَالَ لَهُ عُمَرُ فَإِنَّهُ الآنَ وَاللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآنَ يَا عُمَرُ))

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin Hishaam (رضي الله عنه):  Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ameushika mkono wa ‘Umar bin Al-Khattwaab. ‘Umar akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, hakika wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko kitu chochote isipokuwa nafsi yangu.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana, (haiwezekani hivyo). Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mpaka niwe kipenzi zaidi kwako kuliko nafsi yako.” ‘Umar (رضي الله عنه)  akamwambia:  Basi kwa sasa Wa-Allaahi wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko nafsi yangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hivi sasa ee ‘Umar (umekuwa Muumini wa kweli).” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللّه عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ )) متفق عليه

Imesimuliwa na Anas bin Maalik kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

Share