024-Hiswnul-Muslim: Du’aa Baada Ya Tashahhud Kabla Ya Salaam

Hiswnul-Muslim

024-Du’aa Baada Ya Tashahhud Kabla Ya Salaam

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[55]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر، وَمِـنْ عَذابِ جَهَـنَّم، وَمِـنْ فِتْـنَةِ المَحْـيا وَالمَمـات، وَمِـنْ شَـرِّ فِتْـنَةِ المَسيحِ الدَّجّال

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min ‘adhaabil qabri, wa min ‘adhaabi jahannam, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil-Masiyhid-dajjaal

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako na adhabu za kaburi, na adhabu ya Jahannam, na fitna ya uhai, na (fitna) ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal[1].

 

 

 

[56]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِـنْ عَذابِ القَـبْر، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المْسيحِ الدَّجّـال، وَأَعـوذُ بِكَ مِـنْ فِتْـنَةِ المْحْـيا وَالمْمـات. اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِكَ مِنَ المْأْثَـمِ وَالمْغْـرَم

 

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min ‘adhaabil qabri, wa a’uwdhu bika min fitnatil Masiyhid-dajaal wa a’uwdhu bika min fitnatil mahyaa wal mamaat, Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal ma-athami wal maghrami

 

Ee Allaah!  Hakika mimi najikinga Kwako na adhabu ya kaburi, na najikinga Kwako na fitna ya Masihid-dajjaal, na najikinda Kwako na fitna ya uhai na (fitna) ya mauti, Ee Allaah, hakika mimi najikinda Kwako kutokana na dhambi na deni[2]

 

 

 

 [57]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم

Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman kathiyraa, walaa  yaghfirudh-dhunuwba illa Anta, faghfir liy maghfiratan min ’Indika warhamniy, Innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym

 

Ee Allaah hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, na haghufurii (yeyote) madhambi ila Wewe, basi nighufurie maghfira kutoka Kwako, na Unirehemu, hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu[3].

 

 

[58]

 

اللّهُـمَّ اغْـفِرْ لي ما قَدَّمْـتُ وَما أَخَّرْت، وَما أَسْـرَرْتُ وَما أَعْلَـنْت، وَما أَسْـرَفْت، وَما أَنْتَ أَعْـلَمُ بِهِ مِنِّي أَنْتَ المُقَـدِّمُ، وَأَنْتَ المُـؤَخِّـرُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْـت

 

Allaahuumaghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’-lantu, wamaa asraftu, wamaa Anta A’-lamu bihi minniy Antal-Muqaddimu wa  Antal-Muakh-khiru laa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah nighufurie niliyoyatanguliza, na niliyoyachelewesha, na niliyoyafanya kwa siri, na niliyoyafanya kwa dhahiri na niliyoruka mipaka, na ambayo Wewe Unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe Ndiye mwenye kutanguliza na Wewe Ndiye mwenye kuchelewesha, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe[4]

 

 

[59]

اللّهُـمَّ أَعِـنِّي عَلـى ذِكْـرِكَ وَشُكْـرِك وَحُسْـنِ عِبـادَتِـك

 

Allaahumma A’inniy ’alaa dhikrika washukrika wahusni ’Ibaadatika

 

Ee Allaah nisaidie kukudhukuru, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu[5].

 

 

 

[60]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعوذُ بِكَ مِنَ البُخْـل، وَأَعوذُ بِكَ مِنَ الجُـبْن، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلى أَرْذَلِ الـعُمُر، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَـةِ الدُّنْـيا وَعَـذابِ القَـبْر.

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika minal-bukhli, wa a’uwdhu Bika minal-jubni, wa a’uwudhu Bika min an uradda ilaa ardhalil-’umri, wa a’uwudhu Bika min fitnatid-duniyaa wa ’adhaabil-qabr

 

Ee Allaah najikinga Kwako kutokana na ubakhili, na najikinga Kwako kutokana na uwoga, na najikinga Kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na najikinga Kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi[6].

 

 

 

[61]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وأَعوذُ بِـكَ مِـنَ الـنّار

 

Allaahumma inniy as-alukal-Jannah wa a’uwdhu Bika minan-naar

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga Kwako kutokana na Moto[7]

 

 

 

[62]

 

اللّهُـمَّ بِعِلْـمِكَ الغَـيْبِ وَقُـدْرَتِـكَ عَلـى الْخَلقِ, أَحْـيِني ما عَلِـمْتَ الحـياةَ خَـيْراً لـي، وَتَوَفَّـني إِذا عَلِـمْتَ الوَفـاةَ  خَـيْراً  لـي، اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْـأَلُـكَ خَشْيَتَـكَ في الغَـيْبِ وَالشَّهـادَةِ، وَأَسْـأَلُـكَ كَلِمَـةَ الحَـقِّ في الرِّضـا وَالغَضَـب، وَأَسْـأَلُـكَ القَصْدَ في الغِنـى وَالفَقْـر، وَأَسْـأَلُـكَ  نَعـيماً لا يَنْفَـد، وَأَسْـأَلُـكَ قُـرَّةَ عَيْـنٍ لا تَنْـقَطِعْ  وَأَسْـأَلُـكَ الرِّضـا بَعْـدَ القَضـاء، وَأَسْـأَلُـكَ بًـرْدَ الْعَـيْشِ بَعْـدَ الْمَـوْت، وَأَسْـأَلُـكَ لَـذَّةَ النَّظَـرِ إِلـى وَجْـهِكَ وَالشَّـوْقَ إِلـى لِقـائِـك، في غَـيرِ ضَـرّاءَ مُضِـرَّة، وَلا فِتْـنَةٍ مُضـلَّة، اللّهُـمَّ  زَيِّـنّا بِزينَـةِ الإيـمان، وَاجْـعَلنا هُـداةً مُهْـتَدين

 

Allaahumma bi ‘ilmikal-ghaybi wa Qudratika ‘alalkhalqi, Ahyiniy maa ‘alimtal-hayaata khayralliy, wa Tawaffaniy idhaa ‘alimtal-wafaata khayralliy. Allaahumma inniy as-aluka khashyataka filghaybi wash-shahaadati, wa as-aluka kalimatal-haqqi fir-ridhwaa walghadhwabi, wa as-alukal qaswda fil-ghinaa walfaqri, wa as-aluka na’iyman laa yanfadu, wa as-aluka qurrata ‘aynin laa tanqatwi’u, wa as-alukar-ridhwaa ba’dal-qadhwaai, wa as-aluka bardal-‘ayshi ba’dal-mawti, wa as-aluka laddhatan-nadhwari ilaa Wajhika, wash-shawqa ilaa liqaaika fiy ghayri dhawarraa mudhwirratin walaa fitnatin mudhwillatin. Allaahumma zayyinaa biziynatil-iymaani waj-’alnaa hudaatan muhtadiyna

 

Ee Allaah naomba kwa ujuzi Wako wa ghaibu na uwezo Wako juu Ulivyooumba, nihuishe ikiwa Unajua kwamba uhai ni bora kwangu, na nifishe ikiwa Unajua kuwa mauti ni bora kwangu. Ee Allaah, nakuomba kukuhofu Kwako kwa siri na dhahiri, na nakuomba neno la haki wakati wa furaha na ghadahbu, na nakuomba unifanye wastani (usawa) wakati wa utajiri na umasikini, na nakuomba neema isiyokoma, na kitulizo cha macho kisichokatika, na nakuomba niridhike kwa Uliyonikidhia (majaaliwa), na nakuomba maisha ya kuburudika baada ya mauti, na nakuomba ladha ya kukutazama Wajihi Wako na shauku ya kukutana Nawe, pasi na madhara yanayodhuru au fitna itakayoleta upotofu. Ee Allaah, tupambie kwa kipambo cha imani na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka[8]

 

 

 

[63]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ يا اللهُ بِأَنَّـكَ الواحِـدُ الأَحَـد، الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَدْ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد، أَنْ تَغْـفِرْ لي ذُنـوبي إِنَّـكَ أَنْـتَ الغَفـورُ الرَّحِّـيم

 

Allaahumma inniy as-aluka yaa Allaahu biannakal-Waahidu Al-Ahadu, Asw-Swamadu Alladhiy lam yalid walam yuwlad walam yakun lahu kufuwan ahad, an Taghfiraliy dhunuwbiy Innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba, Ee Allaah kwa vile Wewe ni Mmoja Uliye Pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, Ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unighufurie madhambi yangu hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria Mwenye kurehemu[9].

 

 

 

 [64]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَـمْدُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَـريكَ لَـكَ المَنّـانُ يا بَديـعَ السَّمواتِ وَالأَرْضِ يا ذا الجَلالِ وَالإِكْـرام، يا حَـيُّ يا قَـيّومُ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وَأَعـوذُ بِـكَ مِنَ الـنّار

 

Allaahumma inniy as-aluka bianna Lakal-Hamdu laa ilaaha illaa Anta Wahdaka laa shariyka Laka Al-Mannaanu yaa Badiy’as-samaawaati wal-ardhwi, yaadhal-Jalaali wal Ikiraami, yaa Hayyu yaa Qayyuwmu, inniy as-alukal-Jannata wa a’uwdhu bika minan-naari

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba, kwa vile Himdi ni Zako, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, hali ya kuwa Peke Yako huna mshirika, Mwingi wa Kuneemesha. Ee Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Ee Mwenye Utukufu na Ukarimu, Ee Uliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, hakika mimi nakuomba Jannah, na najikinga Kwako kutokana na Moto[10]

 

 

 

[65]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّـي أَشْـهَدُ أَنَّـكَ أنْـتَ اللهُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـت، الأَحَـدُ الصَّـمَدُ الَّـذي لَـمْ يَلِـدْ وَلَمْ يولَـدْ، وَلَمْ يَكـنْ لَهُ كُـفُواً أَحَـد.

Allaahumma inniy as-aluka bianniy ash-hadu Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illaa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu Alladhiyy lam yalid walam yuwlad walam yakun lahu kufuwan ahad

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba kwa vile nashuhudia  kwamba hakika Wewe ni Allaah hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, hali ya kuwa Pekee, Mwenye Kutegemewa kwa haja zote, Ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote[11]

 

 

 


[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (2/102), Muslim (1/412), na tamshi la Muslim

[2]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy (1/202), Muslim (1/412) na tamshi lake.

[3]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما) - Al-Bukhaariy (8/168),  Muslim (4/2078) 

[4]Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه) - Muslim (1/534)

[5]Hadiyth ya Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2/86), An-Nasaaiy (3/53) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/284)

[6]Hadiyth ya Sa’iyd bin Abi Waqqaasw (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/35) [2822]

[7]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd [792] na ibn Maajah na angalia: Swahiyh ibn Maajah (2/328)

[8]Hadiyth ya ‘Ammaar bin Yaasir (رضي الله عنه) - An-Nasaaiy (4/54-55), Ahmad  (4/364) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh An-Nasaaiy (1/280/281)

[9]Hadiyth ya Mahijan bin Al-Arda’ (رضي الله عنه) - An-Nasaaiy kwa tamshi lake (3/52), Ahmad (4/238) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh An-Nasaaiy (1/280)

[10]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) Imetaja mwisho wa Hadiyth:

((لَقَدْ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الْأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى))

((kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Tukufu ambalo Anapoombwa kwalo Anaitikia na Anapotakwa kwalo jambo hutoa)) - Ahlus-Sunan; Abu Daawuwd [1495], An-Nasaaiy (3/52), ibn Maajah [3858] na taz Swahiyh ibn Maajah (2/329)

[11]Hadiyth ya Buraydah bin Al-Huswayb Al-Aslamiyy (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2/62) [1493], At-Tirmidhiy (5/515) [3475], Ibn Maajah (2/1267) [3857], Ahmad (5/360), na angalia: Swahiyh ibn Maajah (2/329) na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/163)

 

 

Share